Natafuta kampuni ya kunikopesha bajaji

Kama upo Dar, nenda Mwenge mpakani. Kuna kampuni inaitwa WATU ambayo inatoa mikopo ya boda na bajaji. Vigezo vyao ni:
  1. Uwe na kitambulisho cha taifa, leseni au kadi ya mpiga kura
  2. Uwe na TIN (namba ya utambulisho wa mlipa kodi)
  3. Uwe na mdhamini mmoja
  4. Kianzio cha 300,000 hadi laki 7
  5. Barua kutoka serikali ya mtaa
Na kwa bajaji, vigezo ni hivyo hivyo isipokuwa kianzio ni kati ya 1,000,000 hadi 1,500,000.
 
Wewe mtu hata haukumfahamu, akakupa tu bajaji. Ungeanza kwanza na baiskeli ili kujenga imani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…