Natafuta kampuni ya uchimbaji visima

Mimi nimechimbiwa kisima. Kwanza ilianza survyey kujua kama maji yapo na yapo mbali kiasi gani. Majibu yakaonyesha yapo kuanzia mita 60. Bei ya kuchimba mita moja ilikuwa 60 000. Nikakubali. Akachimba na maji yakapatikana m65. Yakapimwa wingi.kiwango cha chumvi na ubora. Baada ya hapo nikapewa aina za pump na bei zake na kiwango cha ubora. Nikafunga. Dawasco ikawa ni kwaheri.
 
Haya ndio maneno tunataka kuona, sio porojo za mwanzo.

Vipi kwa nje ya Dar mfano ameneo kama Mkuranga au Rufiji mbayo ni pembezoni mwa mto bei zenu zinakuaje maana kuna fununu hauzidi mita hamsini ushakutana na maji
 
Mkuu hivi visima vinatoa maji full year??

Vipi maji yake ni mengi kiasi naweza kumwagilia bustani ya ukubwa wa hekari moja??

Vipi kuhusu chumvi maana ukanda huu wa pwani maji ni chumvi mno, au walitoboa mwamba wa maji baridi??
 
Mimi naitwa jackson lyimo akar jack pemba nifundi a!c mzuri sana 2tafutane 2ongee
 
Sasa ni kipi kilichokuwa kikikufanya udengue kutaja bei zako? Hadi usikie kuna alternative ya mchina?
 
Maswi drilling ni wachimbaji wa visima vya aina yote, ni wazoefu na wanawatalam waliobobea katika shughuli zao, wana mashine za kisasa. Pia wana matawi nyanda zote kuanzia, kanda ya ziwa, dsm(ofisi ipo kariakoo), moshi, iringa, na mtwara, wasiliana nao kupitia hapa maswidrilling.com/index.html
 
Nipo pugu kigogo fresh! Nahitaji kampuni ya kunichimbia kisima kirefu. Nijulishe gharama zake. Tuwasiliana no 0718412041

Maswi drilling ni wachimbaji wa visima vya aina yote, ni wazoefu na wanawatalam waliobobea katika shughuli zao, wana mashine za kisasa. Pia wana matawi nyanda zote kuanzia, kanda ya ziwa, dsm(ofisi ipo kariakoo), moshi, iringa, na mtwara, wasiliana nao kupitia hapa maswidrilling.com/index.html
 
Baba yangu yuko Mwanza ana kampuni yake inaitwa GEWECO( ground waters and wells construction limited) pia ana masters ya taaluma hii toka Auckland university pala New zealand.

Ana uzoefu wa kutosha na shughuli hizi na bei zake ni nafuu sana kwani anafanya miradi mingi kwa ajili ya manufaa ya jamii. Namba yake ni 0754 593 401.

Kila la kheri wandugu.
 
Nitakupaje bei wakati haijulikani unataka kuchimba mita ngapi

Mbona hapa umeweka mita na bei mwenyewe, kimeharibika nini? Narudia tena watanzania acheni ujanjaujanja. Hiyo karne imekwisha siku hizi hata bidhaa zilizopo Marekani, China Japan wanaweka bei. Why not in Tanzania?
 
Haya ndio maneno tunataka kuona, sio porojo za mwanzo.

Vipi kwa nje ya Dar mfano ameneo kama Mkuranga au Rufiji mbayo ni pembezoni mwa mto bei zenu zinakuaje maana kuna fununu hauzidi mita hamsini ushakutana na maji

Bei ni hizo hizo kwa maeneo yote ya pwani unaongeza cost za usafiri, malazi labda na kubadilika kwa bei ya mafuta kama ni tofauti sana na jijini
 
Mwaga bei kwa mita unachimba sh.ngapi acha porojo unapiga picha mashine za watu alafu unaanza porojo!!!na kufanya survey sh. Ngapi???🙁

alichosema mdau ni sahihi kabisa bei iatokana na eneo hawezi kutaja bei bila kufanya survey na kujua maji yako umbali gani toka usawa wa ardhi ameongea kitaalam sana huwezi kutaja bei bila kufika wala kujua eneo lenyewe vp kama maji yapo mita 100 chini ya ardhi au mita 20 bei si zitatofautiana
 
Kuna jamaa wametoka kunichimbia mita 130 sala sala, nimewapa 7.5 mil. Including pump ya 1.5hp. Nimepata maji mengi sana na masafi sana hayana chumvi. Dawasco bye bye.
 
Kuna jamaa wametoka kunichimbia mita 130 sala sala, nimewapa 7.5 mil. Including pump ya 1.5hp. Nimepata maji mengi sana na masafi sana hayana chumvi. Dawasco bye bye.

vp walifanya survey kabla??weka mawasiliano yao mkuu!
 
nadhani huyu anafaa kwani anasifa za ziada...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…