Natafuta kampuni ya uchimbaji visima

Natafuta kampuni ya uchimbaji visima

Maswi drilling ni wachimbaji wa visima vya aina yote, ni wazoefu na wanawatalam waliobobea katika shughuli zao, wana mashine za kisasa. Pia wana matawi nyanda zote kuanzia, kanda ya ziwa, dsm(ofisi ipo kariakoo), moshi, iringa, na mtwara, wasiliana nao kupitia hapa maswidrilling.com/index.html

Wewe ndo mwenye kampuni au unafanya kazi huko?
 
Hii ya Kibiti hata mi naisubiria, ukiipata nishtue mkuu!
Please!

Kuna jamaa anachimba visima vya pete na vya kuchoronga manually na garama zake ni nafuu kwa kweli kanishangaza, nitakutumia namba zake uongee nae
 
Wewe ndo mwenye kampuni au unafanya kazi huko?

Hapana mkuu sina hata uhusiano nao bali niliwahi kushuhudia kazi zao huko magu, hivo nikashawishika kutaka kufahamu zaidi kuhusu wao ndo nkapata hiyo website yao
 
Mimi nimechimbiwa kisima. Kwanza ilianza survyey kujua kama maji yapo na yapo mbali kiasi gani. Majibu yakaonyesha yapo kuanzia mita 60. Bei ya kuchimba mita moja ilikuwa 60 000. Nikakubali. Akachimba na maji yakapatikana m65. Yakapimwa wingi.kiwango cha chumvi na ubora. Baada ya hapo nikapewa aina za pump na bei zake na kiwango cha ubora. Nikafunga. Dawasco ikawa ni kwaheri.

Survey kwa bei gani mkuu?
 
Tawa driller ni mabingwa wa uchimbaji visima virefu na vifupi pia tunafanya ground water survey kwa bei rahisi tu kwa walioko dar es salaam tunachimba shillingi 60000 kwa mita moja na pia tunafanya ground water survey kwa shillingi 250000 kwa waliopo dar es salaam lakini pia tunafanya kazi hadi mikoani
Kwa mawasiliano piga simu namba 0628080096
 
Huduma Vp Zinaendelea
Kwa Morogoro Kingolwira Naweza Kupata Wataalam
 
Tawa driller ni mabingwa wa uchimbaji visima virefu na vifupi pia tunafanya ground water survey kwa bei rahisi tu kwa walioko dar es salaam tunachimba shillingi 60000 kwa mita moja na pia tunafanya ground water survey kwa shillingi 250000 kwa waliopo dar es salaam lakini pia tunafanya kazi hadi mikoani
Kwa mawasiliano piga simu namba 0628080096

Ndugu mtaalamu, naomba kuuliza je inawezekana kupata maji yasiyoyachumvi kwa maeneo ambayo asilimia 95 ya visima vinatoa maji chumvi?. Mfano mzuri ni chunya-mbeya.
 
Ndugu mtaalamu, naomba kuuliza je inawezekana kupata maji yasiyoyachumvi kwa maeneo ambayo asilimia 95 ya visima vinatoa maji chumvi?. Mfano mzuri ni chunya-mbeya.
acha Tungoje Majibu Maana Swali Zuri Sana
 
Back
Top Bottom