Watu wengine bana....mnajifanya kutoa ushauri wakati kutoa ushauri hamjui!!! Wataalamu wa kutoa ushauri ni lazima tuisome saikolojia ya mwomba ushauri kwanza; nyie vp?! Jamaa amesema yeye ni mgeni hapa Dar lakini sio mgeni wa hapa JF. Anafahamu fika nini a-post wapi.....mnazani amekosea?! Amekuja jukwaa la malavidavi na kuomba ushauri ni kanisa gani aende...nyie mnamwambia habari za Kakobe, Lwakatare sijui na akina sijui...!!! Kutokana na utaalamu wangu, yeye anatafuta kanisa ambalo baada ya sala, waumini wanafumba macho na kunena kwa vitendo; ala! Kwani hamjui kwamba ni matokeo ya dhambi ndipo mwanadamu akaanza kuvaa nguo?! Ina maana mmesahau ni baada ya Braza Adam kumega ki2 ndipo wakajishtukia na kuamua kutupia gwanda?! Hadi mtafuniwe kila ki2!!! Mkuu, ukilipata nami nitonye nikajoin!