Fanya kazi kaka jiajiri mwenyewe wewe unafanya graphics halafu kuajiriwa, mbona uchumi unao halafu unaukalia, kama. Huna vyeti sio mwisho wa maisha, kuna watu kibao wana vyeti lakini output zero na hiyo ni kwenye fani zote, si unaona jinsi wasomi wetu wanavyo sign mikataba ya ajabu na mivyeti yao. Unahitaji vitu vitatu tu kufanikiwa, Confidence, Competence & Commitment. Nimesoma mtu mmoja amekuita kanjanja achana nae, mimi ni designer pia sina cheti chochote wala sijawahi kusoma shule yoyote ya graphics, lakini nimefanya kama production supervisor kwenye media houses kubwa nikiongoza timu za watu not less than 20 kwenye studio, na nimefanya kazi nzuri huku nikiwa panelist kwenye interviews za hao wenye vyeti, sasa hivi nimejiajiri. Kaza buti mvuagamba.