Natafuta kazi, nina Bachelor ya HR 2014 na Masters ya HR 2022

lordboy

Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
19
Reaction score
51
Wakuu naombeni mwenye link yoyote ya kunisaidia kupata kazi anisaidie.

Nina bachelor ya Hr 2014 na masters ya hr 2022, nimekomaa kusaka ajira mara kadhaa bila kufanikiwa, nilipomaliza chuo nilipiga JKT miaka 3 Magu akatumwaga mtaani bila ajira, nikakimbizana huku na huko nikaangukia kwenye biashara ya kuuza pembejeo za kilimo kanda ya ziwa kampuni ikayumba nikarudi Arusha.

Huku Arusha nikaingia kwenye mambo ya utalii kufanya town tours na trips ndogo ndogo japo mara moja moja nafanya safaris nikiotea magroup ya wageni naandaa safari nzima na naenda nao, nika rent nyumba nikafungua hostel nikawa napata wageni kadhaa na host lakini kwa hela kidogo sana na wengi ni volunteers ila nilikuja kushindwa kwa sababu ya process za registration na kodi na gharama zingine nyingi.

Sina connection ya watu wazito nimejaribu ku share huku maana naona stress inaweza kunipeleka pabaya bora nishauriwe mawili matatu na wadau humu.
 
Bachelor ulisoma Chuo gani?Masters ulisoma Chuo gani?na inakuaje ujitolee JKT miaka mitatu kisha ushindwe kuingia kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Polisi,TAKUKURU,Uhamiaji,Zimamoto na JWTZ?
 
Wakuu naombeni mwenye link yoyote ya kunisaidia kupata kazi anisaidie.

Nina bachelor ya Hr 2014 na masters ya hr 2022,
Wakati mwingine unapotaja qualification anza na Highest to lowest. Mfano ulitakiwa uanze na Masters then Bachelor Degree. Watu wasionkuwa na muda wa kusoma akishaanza na bachelor wala haendelei. Lakini akishakuta Masters atataka kujua Bachelor umesoma nini
 
kwel mkuu nimekosea hapo, kichwa hakikua sawa kabisa
 
Back
Top Bottom