Natafuta kazi, nina Bachelor ya HR 2014 na Masters ya HR 2022

Bachelor ulisoma Chuo gani?Masters ulisoma Chuo gani?na inakuaje ujitolee JKT miaka mitatu kisha ushindwe kuingia kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Polisi,TAKUKURU,Uhamiaji,Zimamoto na JWTZ?
Bach ilikua Tumaini university na master’s ni Uhasibu arusha.
Magu alituweka kwa ahadi kibao za ajira baadae akatumwaga kama unakumbuka alisema amesha apisha ma ofisa wa kutosha na hana mpango wa ajira tena, baada ya mwezi tukatolewa op magu wote japo wengine wenye mibuyu mizito walibaki na silaumu kwa sababu sikua na connection hvyo haikua riziki yangu
 
Yani ungeendelea kukomaa na sector ya utalii ingekutoa maana tayali una experience nayo alafu kwann tena ukaenda kusoma masters ya human resource wakati una degree yake ambayo haijakupa impact yoyote mtaani?
sijakata tamaa kabisa nimekutana na mdau mmoja tunaanza tena kusogea mbele, bado nina imani
 
Wakuu naombeni mwenye link yoyote ya kunisaidia kupata kazi anisaidie.

Nina bachelor ya Hr 2014 na masters ya hr 2022, nimekomaa kusaka ajira mara kadhaa bila kufanikiwa, nilipomaliza chuo nilipiga JKT miaka 3 Magu akatumwaga mtaani bila ajira, nikakimbizana huku na huko nikaangukia kwenye biashara ya kuuza pembejeo za kilimo kanda ya ziwa kampuni ikayumba nikarudi Arusha.

Huku Arusha nikaingia kwenye mambo ya utalii kufanya town tours na trips ndogo ndogo japo mara moja moja nafanya safaris nikiotea magroup ya wageni naandaa safari nzima na naenda nao, nika rent nyumba nikafungua hostel nikawa napata wageni kadhaa na host lakini kwa hela kidogo sana na wengi ni volunteers ila nilikuja kushindwa kwa sababu ya process za registration na kodi na gharama zingine nyingi.

Sina connection ya watu wazito nimejaribu ku share huku maana naona stress inaweza kunipeleka pabaya bora nishauriwe mawili matatu na wadau humu.
Nenda baa ya jirani na unapokaa ukajitolee (volunteer)
 
Pole sana mkuu. Kwanini usiendelee na utalii? Uzoefu unao na wateja unapata endelea nao mdogo mdogo kama vibali na taratibu nyingine ni changamoto kwa sasa fanya kuwalink wateja wako na makampuni, baadhi hutoa pesa kiasi fulani kwa wanaowaletea watalii.
nilifanya sana hizo na ndio nilipata ka mtaji wa kufungua hostel, ila juzi kati nimekutana na neema kidogo naona hali si mbaya.
Tatizo ni kuzungukana, biashara za partnership huku kwetu ni changamoto sana, ukim link mtu na mgeni ndio mwisho wa ww kuwa na uhusinao na huyo mgeni kwa maneno atakayo jazwa
 
Wakuu naombeni mwenye link yoyote ya kunisaidia kupata kazi anisaidie.

Nina bachelor ya Hr 2014 na masters ya hr 2022, nimekomaa kusaka ajira mara kadhaa bila kufanikiwa, nilipomaliza chuo nilipiga JKT miaka 3 Magu akatumwaga mtaani bila ajira, nikakimbizana huku na huko nikaangukia kwenye biashara ya kuuza pembejeo za kilimo kanda ya ziwa kampuni ikayumba nikarudi Arusha.

Huku Arusha nikaingia kwenye mambo ya utalii kufanya town tours na trips ndogo ndogo japo mara moja moja nafanya safaris nikiotea magroup ya wageni naandaa safari nzima na naenda nao, nika rent nyumba nikafungua hostel nikawa napata wageni kadhaa na host lakini kwa hela kidogo sana na wengi ni volunteers ila nilikuja kushindwa kwa sababu ya process za registration na kodi na gharama zingine nyingi.

Sina connection ya watu wazito nimejaribu ku share huku maana naona stress inaweza kunipeleka pabaya bora nishauriwe mawili matatu na wadau humu.
Binafsi nakushauri ujitafte kwa kazi zako Binafsi kama mtaji unao angalia fursa mikoa mingine, Hususani mkoa wa mtwara kwa sasa naona kuna fursa huko lakini pia kuna mji unaitwa katoro kwa Tanzania kama huwezi pambana Dsm hizo sehemu mbili nadhani ukikomaa unatoka..
Kazi siku hizi kama huna mtu wa kukushika mkono ni ngumu kupata jitafute mdogomdogo utatoboa... Epuka mademu au wanawake....
 
nilishafanya kazi kwenye restaurant kadhaa na bar kadhaa, nimeshapika sana pizza na bbq mkuu, hata kitimoto niko fit lakini kuna kukata tamaa flani iliniingia na kukatishwa tamaa pia
Sasa Mkuu kama umepita kote huko bado unatafutwa ajira? Anza na jiko la kitimoto. mhudumu weka lishangazi
 
Sasa Mkuu kama umepita kote huko bado unatafutwa ajira? Anza na huko la kitimoto
faida ni kufungua lako mwenyewe, napambana ipo siku ntaweka goli, bro sasa hv nina pumzi kidogo ila siku nimepost hii kitu kaka huwez amini nilikua kwenye hali mbaya sana, Nimeona umuhimu wa ku share jambo na watu hata ushauri tu huwa unasaidia sana na kutia moyo mno
 
nilifanya sana hizo na ndio nilipata ka mtaji wa kufungua hostel, ila juzi kati nimekutana na neema kidogo naona hali si mbaya.
Tatizo ni kuzungukana, biashara za partnership huku kwetu ni changamoto sana, ukim link mtu na mgeni ndio mwisho wa ww kuwa na uhusinao na huyo mgeni kwa maneno atakayo jazwa
Pesa ndio chanzo cha hayo yote inahuzunisha sana.
 
faida ni kufungua lako mwenyewe, napambana ipo siku ntaweka goli, bro sasa hv nina pumzi kidogo ila siku nimepost hii kitu kaka huwez amini nilikua kwenye hali mbaya sana, Nimeona umuhimu wa ku share jambo na watu hata ushauri tu huwa unasaidia sana na kutia moyo mno
1. Mkuu usituone tunaendesha mandinga tumeyapitia hayo maisha.

2. Niliwahi kwenda kuuza ice cream uwanja wa Taifa siku za mechi kama mwezi hivi baadae nikasepa na ice cream pamoja na lile container 'deli' la ice cream tajiri hakuniona tena kmmk
 
Uza kitimoto. Mafuta tumia ya Transfoma faida mara 10.
 
1. Mkuu usituone tunaendesha mandinga tumeyapitia hayo maisha.

2. Niliwahi kwenda kuuza ice cream uwanja wa Taifa siku za mechi kama mwezi hivi baadae nikasepa na ice cream pamoja na lile container 'deli' la ice cream tajiri hakuniona tena kmmk
Nikupambana.kwann ulisepa na del?
 
Back
Top Bottom