Natafuta kazi ya jikoni - kuuza chipsi, kuku, supu n.k

Mimi kuna sehemu kuna Bar ipo mbezi kuna Jiko lakini halina mtu. kama una mtaji nikuunganishe hapo uende ukapige hela.

Unaweza kuuza Chips, Kongoro, Kuchoma nyama lakini pia lipo lingine hapo hapo la Kitimoto
Naomba niunganishe mkuuu au mwambie mtoa mada ataniambia nahitaji hilo jiko.
 
Umemaliza akutafute
 
Unataka kulipwa Tsh ngapi?
 
Wakuu bado nafatilia FURSA ya jikoni bado sijapata .

Nipo DSM kibamba naomba MTU yeyote mwenye kazi au anatafuta kijana mwaminifu anijulishe.

Nahitaji kazi Sana wakuu.

Mimi nipo vizuri katika haya maeneo

Biashara ya chips
Kuuza na kuandaa chips
Kuku wa kukaanga
Supu ya kuku ,mbuzi na n'gombe
Supu ya kongoro.


Pia tunaweza kupanua biashara kwa kuuza na chakula kama ugali, wali na ndizi.


Napatikana Muda wote kuanzia sasa 24/7
 
Ungekuwa Mwanza hii coment yangu ingekuwa mwisho wa uzi wako.
 
Nafikiri wanalipa kwa siku elfu tano
Wakuu niwasaidie kitu, kwenye kuanza biashara yoyote ile usifunge mkataba mnono na mwenye bar au nyumba. mwanzoni ikibidi mgrind to the maximum ukifanikiwa kwa hilo baadae utakuja kuishukuru hii comment yaani mfano hapo nimeona jiko per day 5k wewe funga nae siku 30 tu za matazamio kwa hiyo hiyo 5k yake kwanza, kisha ukijiridhisha na consumption ya bidhaa yako unafunga nae mkataba wa 2.5k per day..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…