Natafuta kazi yoyote ya kutumia nguvu au akili

Habari wakuu!

Mimi Ni mwanafunzi(22) wa mwaka wa Pili chuo Fulani hapa Dar es salaam!
Nasoma Bachelor Degree in Gender and development.

Kutokana na Hali ya maisha kuwa mbaya Sana kwa upande WANGU,
Nilimeamua kuja mbele yenu ndugu zangu, kuomba kazi yoyote ili niwe na chanzo chochote Cha mapato Rakini pia niweze kuendesha maisha Yangu Mana Nina andamwa na Kodi ada nk

Ukosefu wa pesa awamu hii ya muhula wa kwanza ndio imenifanya kutofanya mthiani wa Mwisho (UE) kwa sababu ya kukosa Ada. Hivyo najiandaa na Special September uku nikitafuta Ada ya semester 2

Hivyo naombeni mnisaidie kuniunganisha kwa Namna Yoyote ili na Mimi nianze kupambana.

Uzuri wa ratiba za chuoni kwetu, naweza kujigawa na nikafanya vizuri pande zote mbili.

Aina ya kazi ninazohitaji.
1. Ulinzi(night shift)
2. Stationary
3. Bodaboda na Bajaj kwa mkataba
4.petrol station (night shift)

Na kazi ingine yoyote itakayo patikana nipo Tayari kuifanya.

Uwezo Wangu.
1.Ninaweza kufanya kazi kwa uaminifu Mkubwa
2.Kushirikiana vizuri na Team yangu katika kazi
3.Nina uwezo Mkubwa wa kutatua matatizo (critical problem solving skills)
4.ujuzi wa kompyuta

Naomba Kama Kuna mtu Ana kazi yoyote Ile mawasiliano Yangu 0784312904
 
Hii kazi mbona watu hatufuati tena vigezo na masharti ?

Sasa kama mchana kutwa unahangaika kufanya mengine, si usiku utakuja kulala na sio kulinda ?
Samahani mkuu nikuulize swali?
Wale walinzi wote ambao wanakuwa na shift za usiku! Mchana kutwa huwa wanashinda wamelala usiku wanaenda kukesha au huwa wanafanya Mambo Yao? Na usiku wanaenda kulinda??

Nina wafahamu walinzi wengi ambao mchana huwa katika kazi zao za Bodaboda na usiku wanaenda kulinda.

Suala la kulala au kutolala kazini Ni suala la kiulinzi zaidi mkuu[emoji2][emoji2]
 
Naam Je hawa wote wanafuata masharti na vigezo vya hii kazi ? Takupa Hadithi ambayo niliwahi kuisikia japo sina uhakika kama ni hekaya au ukweli...

Alikuwepo mlinzi mmoja ambaye alikuwa ana tabia ya kupiga usingizi kwenye lindo..., siku moja bosi wake akaamua amkomoe usiku ulipofika kuna bidhaa zilikuwa zinawekwa hapo barazani; Bosi akachukue hizo bidhaa, upinde na rungu la mlinzi na kuviweka ndani, alafu akarudi zake kupiga usingizi....

Baada ya masaa wakasikia kelele kutoka nje wakakuta mlinzi amejaa vumbi na kutoka damu usoni..., kumuuliza vipi akadai wamekuja wadau wakampiga ma kitu kichwani akazimia na wameondoka na mshale wake na vitu vilivyokuwepo hapo barazani (kumbe jamaa baada ya kuamka na kukuta kuna vitu havipo akaamua kujigonga kichwa ukutani na kujichafua na kutunga story ya uongo....

Kilichofuata ni kupoteza kazi yake....
 
[emoji1787][emoji1787] Hatari mkuu! Ila hizo Ni changamoto tu, maisha ndio yanatufanya tuwe Hivyo, Kama ningekuwa na maisha mazuri huu Uzi usinge uona mkuu
 
Kama unaweza kuzungumza mbele za watu bila uoga wala wasiwasi basi ni vyema ukafikiria kugombea nafasi za uongozi ndani ya CCM si unajua mwaka huu ni mwaka wao wa uchaguzi
Sijui kwanini nimejikuta nacheka mpaka machozi kwenye uzi serious kama huu!
 
Kuna mtu hapo juu natarajia kuwasiliana nae mkuu.
Mkuu, nimejaribu kukutumia PM nimeshindwa/inashindikana, kama inawezekana unaweza nitumia hata "empty PM/PM tupu" iliniweze kukujibu/kuwasiliana kwa namna hiyo.
Asante.
 
Habari wakuu!

Mimi Ni mwanafunzi(22) wa mwaka wa Pili chuo Fulani hapa Dar es salaam!
Nasoma Bachelor Degree in Gender and development.

Kutokana na Hali ya maisha kuwa mbaya Sana kwa upande WANGU,
Nilimeamua kuja mbele yenu ndugu zangu, kuomba kazi yoyote ili niwe na chanzo chochote Cha mapato Rakini pia niweze kuendesha maisha Yangu Mana Nina andamwa na Kodi ada nk

Ukosefu wa pesa awamu hii ya muhula wa kwanza ndio imenifanya kutofanya mthiani wa Mwisho (UE) kwa sababu ya kukosa Ada. Hivyo najiandaa na Special September uku nikitafuta Ada ya semester 2

Hivyo naombeni mnisaidie kuniunganisha kwa Namna Yoyote ili na Mimi nianze kupambana.

Uzuri wa ratiba za chuoni kwetu, naweza kujigawa na nikafanya vizuri pande zote mbili.

Aina ya kazi ninazohitaji.
1. Ulinzi(night shift)
2. Stationary
3. Bodaboda na Bajaj kwa mkataba
4.petrol station (night shift)

Na kazi ingine yoyote itakayo patikana nipo Tayari kuifanya.

Uwezo Wangu.
1.Ninaweza kufanya kazi kwa uaminifu Mkubwa
2.Kushirikiana vizuri na Team yangu katika kazi
3.Nina uwezo Mkubwa wa kutatua matatizo (critical problem solving skills)
4.ujuzi wa kompyuta

Naomba Kama Kuna mtu Ana kazi yoyote Ile mawasiliano Yangu 0784312904
Ulipata kazi mkuu?
 
Back
Top Bottom