Natafuta kibarua au kazi elimu yangu form 4

Natafuta kibarua au kazi elimu yangu form 4

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
13,654
Reaction score
8,564
Kama kuna kibarua au kazi yoyote naombeni mnihabarishe ndugu zangu cna elimu kubwa ninayo ndogo ya form 4
 
Kwqa kweli mi ningekushauri utafute namna ya kuanzisha biashara, hata ndogo ndogo maana itakua vigumu upate kazi nzuri inayo lipa na unayo tumika in dignity kwa elimu hiyo. Au labda nikuulize una experience ipi ya kazi maana unaweza kua form 4 zile za kweli za enzi zetu alafu una miaka kumi ya uzoefu kama mtumishi wa uma?
 
Maisha yamenipga wakubwa c unajua hali mbaya hata ya messenger ntafanya
 
Uko wapi? au unaishi wapi? Kuna kazi kibao wala wasikukatishe taamaa, kwa mfano wale wauza vocha na kusajili namba za simu, Wewe zitokee ofsi za wamiliki wa mitandao, uwaombe kazi hata ya kusajili simu au kufanya promotion. Kwa mfano hapa Dodoma nimeona Offisi za Tigo wanahitaji vijana wa kazi kama uko dodoma changamka.

Kazi nyingine, tafuta zinapojengwa nyumba, magorofa, au barabara, kapige kibarua, utakusanya kisha utapata mtaji na kuanzisha shughuli unayoona inafaa kadri ya mtaji ulionao. La kama we ni legelege hutaweza,manake kule hata menyu kuna siku haugongi.

Pia soma mara kwa mara Gazeti la mwanaspoti, huwa wana matangazo madogo madogo ya ajira kwa vijana wa drs la saba na Form four hasa kwa Dar..
 
Dah elimu ya kidato cha nne si ndogo hebu fikiria masomo yote yale tena yanayogusa mambo mengi tu! Mtindo huu utafanya miaka ya mbele mtu mwenye degree moja aseme nina elimu ndogo kutokana na mfumo wa wakati huo! Kipindi tunasoma o level tulikuwa na upeo wa kutosha wakuchambua mambo(kumbuka debate za wakati huo).mimi nilisoma somo la agriculture ambalo lilinisaidia sana kuanzisha bustani za mboga wakati huo! Kwenye agriculture ya o level kuna mambo mengi ya kitaalamu wa mifugo na mimea tulifundishwa tena kwa vitendo! Ile si elimu ndogo!! Ningeweza kabisa kuajiriwa kusaidia maafisa kilimo wenye hata diploma(wapo wachache sana).hivyo basi tufute neno elimu ndogo,tutengeneze ajira za kada tofauti ku accomodate vijana wetu.mfano kazi ya bank teller na customer care lazima afanye mtu mwenye degree? Nchi zilizoendelea mtu haheshimiwi kwa degree zake bali anachofanya!! Tena wasio na hizo degree wanafanya mambo makubwa na ndio wazalishaji wakubwa! Haiwezekani kila mtu awe na degree kama option iliyobaki kuleta maisha bora.pigana Mungu atakusaidia.
W
 
kuna watu walisoma darasa la 8 la enzi zile walitufanyia kazi nzuri tu kuliko hizi degree za havard! Hivi hayati Kawawa mfano unajua alikuwa na elimu gani?
 
Kwqa kweli mi ningekushauri utafute namna ya kuanzisha biashara, hata ndogo ndogo maana itakua vigumu upate kazi nzuri inayo lipa na unayo tumika in dignity kwa elimu hiyo. Au labda nikuulize una experience ipi ya kazi maana unaweza kua form 4 zile za kweli za enzi zetu alafu una miaka kumi ya uzoefu kama mtumishi wa uma?
Tuwape moyo vijana na si kuwaharibu kisaikolojia kuwa elimu zao ndogo wafikirie kidogo pia! Tuwaambie elimu zao ni kubwa tu kama hakufanikiwa kuendelea.wabuni vitu vya kufanya vitavyowasaidia.zamani physics ya form 2 tayari kuna vijana walikuwa wanatengeneza hadi kituo cha kurusha matangazo ya radio! Tubadili lugha tunazozitumia kwa vijana hawa ili wasiishie kuwa vibarua tu.kuna wahindi ni ma chief accountant na form 4 zao! Kijana buni,dhubutu na nidhamu itakutoa tu!!! Akili isiishie kuwa kibarua eti elimu yako ndogo!!
 
nenda g4s pale karibu na moroco jtatu asbh ukiwa na vyeti vyako, cv, birth cert, barua ya utambulisho unaweza pata kazi mdogo wangu!
 
wewe hebu soma..unataka kufanya kazi na iyo form 4 yako shauri zako
 
Back
Top Bottom