Natafuta mafuta ya mkia wa Kondoo kama dawa

Zamazamani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2008
Posts
1,869
Reaction score
787
Wadau,

Nimeambiwa kuwa mafuta ya mkia wa kondoo ikichanganywa na asali ni dawa nzuri ya kifua na mafua hasa kwa watoto wachanga.Ninatafuta sana mafuta ya mkia wa kondoo naombeni mwongozo wadau!!! (kachanga changu kameshatumia sana madawa ya hospitali lakini tatizo linajirudia jirudia )
PS.Kama kuna dawa nyingine ya kiasili hasa kwa watoto wachanga pia maoni yanakaribishwa.

Ahsanteni
 
Kuwa makini mkuu Zamazamani unapomlambisha mtoto mchanga asali, ukikosea ikampalia unaweza kumkosa.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi huwa natumia iliadin kwa mwanangu, huwa inamsaidia (ila ni ya hospitali)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…