Natafuta masoko ya uwakika ya nafaka ndani ya tanzania na nchi Jirani

Natafuta masoko ya uwakika ya nafaka ndani ya tanzania na nchi Jirani

wakusoma21

Member
Joined
Nov 16, 2019
Posts
29
Reaction score
78
Habari za mapambano wanajamvi kama mada ilivyo hapo juuu. Nimekuwa nafanya biashara ya mazao (mahindi, maharage,mpunga,alizeti) kwa mda wa miaka zaidi mitatu yaaani mimi natafuta mzigo vijijini maeneo ya songwe na Rukwa napeleka soko la tunduma mataifani pia soko la mbalizi. Kuna baadhi ya mambo yamenifanya niandike uzi huuu 1. ni changamoto ya kukusanya mazao ayo shambani kwa wakulima kwa sababu ya ushindani watu wanatumia madalali na changamoto ya madalali na baadhi ya wakulima sio waaminifu unawapa hela wanapita nazo na mnaingia kwenye kudaiana. na ukiamua upambane mwenyewe bila kutumia hao madalali unachukua mda mrefu sana kukusanya mzigo. Kwenye hii changamoto nataka nitoke vijijini nianze kununua mzigo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanaleta kwenye miji midogo midogo kama sumbawanga mjini, laela nk na mimi ninunue nipeleke kwenye masoko makubwa kama huko dar na mtukula. Changamoto ya pili niliyoipata ni pale mataifani tunduma mfumo wa madalali hawakulusu ww uongee na mteja wanakuja kukuambia tuuu haya maharage mteja amesema atalipa bei flan unakuta ipo chini hapa kunaupigaji sana pia wameleta mizani na wanakuambia gunia la maharage linasaminishwa kwa kila 118 na hawaweki bayana kilo bei gani. Kutokana na changamoto ndo nimeleta uzi huu mbele yenu kutafuta masoko mazuri. Msaada yoyote anayejua masoko mazuri ya nafaka anaweza kushare kitu ninachoamini ukimsaidia mtu unakuwa umejiwekea azina
 
Yani ulete mzigo sokoni, dalali akupangie bei ? Hataki wewe uongee na mteja direct ? Pia hujui kg bei gani wewe unapewa hela tu ??

Dah,,,, nikiongea nitakufuru !
 
Yani ulete mzigo sokoni, dalali akupangie bei ? Hataki wewe uongee na mteja direct ? Pia hujui kg bei gani wewe unapewa hela tu ??

Dah,,,, nikiongea nitakufuru !
Ni real bro unaambiwa na dalali hao wacongoman wanahasira hasira usisogee kwenye mzigo wanaweza wakazila wasinunue, pale ni Jau sana ila nikapata majibu kutokana na kua mgeni wa soko labla na mtaji mdogo ndo nahisi ilikua ya wao kufanya hivyo ila sizan kama wanafanya hivyo kwa wengine
 
Mbona hujaweka mawasiliano nikipata information za kutosha tunaweza kufanya biashara njoo pm na mawasiliano yako
 
Back
Top Bottom