Natafuta matairi bora

Yes hadi hii June,nimenunua Pirelli kuna muitaliano aliniambia ikisumbua njoo nakurudishia pesa yako yote yupo pale Karibu na SUPER DOLL PUGU ROAD
 
Yes hadi hii June,nimenunua Pirelli kuna muitaliano aliniambia ikisumbua njoo nakurudishia pesa yako yote yupo pale Karibu na SUPER DOLL PUGU ROAD
ni bei gani kwa tairi kwa hizi gari ndogo 14"
 
Kama una ubavu chukua all weather MICHELIN hii kiboko yao, ukishindwa BF Goodrich ila tatizo lake ni mazito
 
Kuna mtu anataka kuniuzia Yokohama 85000/= Nimeogopa! Kweli jamani...
 
Siyo uongo! Pancha siyo kitu cha lazima kwenye gari. Inategemea unatumia barabara zenye hali gani pia. Ukiweka tairi mpya kukaa bila pacha kwa miaka miwili mitatu ni kitu cha kawaida.
So kuongeza upepo kwny tairi ni lazime kuwe kumetokea pancha sio?
 
Nimenunua Pirelli tangu June last year hadi leo haijapata pancha wala kujaza upepo
Nilinunua Pirelli najuta, yaani zimeshaingia misumari tairi 2 kwa wakati tofauti, afadhali ningenunua Michelin ama BFGoodrich.

Yaani hata km 15,000 hazijafikisha na zimetengenezwa mwaka 2018.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top 10 ya matairi bora duniani 2019 (branddirectory.com)
1. Michellin (France)
2. Pirelli (Italy)
3. Continental (Germany)
4. Goodyear (USA)
5. Cooper (USA)
6. BF Goodrich (UK)
7. Dunlop (USA)
8. Bridgestone (Japan)
9. Yokohama (Japan)
10. Hankook (South Korea)

makampuni haya huwa yanabadilishana nafasi mara kwa mara, kwa mtu wa masafa marefu unashauriwa kutumia matairi haya ila mtu wa safari za mjini mjini bado kuna brand nzuri na bei nafuu kama Goodride, Linglong, Triangle nk
 
Yes hadi hii June,nimenunua Pirelli kuna muitaliano aliniambia ikisumbua njoo nakurudishia pesa yako yote yupo pale Karibu na SUPER DOLL PUGU ROAD
Pirelli ni tyre za uhakika zina nyama ngumu na sio laini kama tairi za mchina zile πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…