Natafuta mawasiliano ya kiwanda cha Alaf

Domhome

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2010
Posts
3,198
Reaction score
3,950
Niliwaandikia email (sales@aluminiumafrica.com) hawa jamaa siku ya Ijumaa, 18 Januari 2013 nikitaka kujua bei ya Mabati ya "IT Maxcover" Gauge 28, kwa Mita moja ni kiasi gani? Lakini hadi leo hii hawajanijibu hiyo email yangu. Jana mida ya saa 8 mchana nikapiga simu Ofisini kwao namba: +255 22 286 330 6 ambayo iliita tu kwa muda mrefu bila kupolewa.

Mawasiliano yote haya niliyapata kupitia Website yao:
WELCOME TO ALUMINIUM AFRICA LIMITED WEBSITE (Company Directory)

Kwa anayejua tafadhali anisaidie niweze kujua bei ya mabati hayo kwasasa ni kiasi gani? na Kama hao ALAF wanayo brach pale Dodoma!!
 
Hawauzi kwa mteja mmojammoja,nenda kwa distributors wao,hata kama ukijua price sio utakayouziwa hiyo ni price ya distributors.

hapana ndugu kwa hizo bati alizotaja zinauzwa kiwandan kwa mteja rejareja lakin bei zake ni kwa metres sio bundles
 
Hawauzi kwa mteja mmojammoja,nenda kwa distributors wao,hata kama ukijua price sio utakayouziwa hiyo ni price ya distributors.
Asante kwa ushauri Mkuu. Ila nadhani hata wao walipaswa kunitajia huyo distributors wao kwa ama pale Dodoma au pengine hata Dar-es-Salaam. Maana hata kama hawauzi nadhani basi walipaswa kunipa majibu haya ulonipa wewe.

Asante Kiongozi!
 
hapana ndugu kwa hizo bati alizotaja zinauzwa kiwandan kwa mteja rejareja lakin bei zake ni kwa metres sio bundles
Na ndo maana nikawasiliana nao moja kwa moja, kwani hata mimi nilikuwa nafahamu hivyo! asante mkuu!
 
Ingia kwenye website yao click distributors hapo utaletewa ramani ya tz then click mkoa uliopo watakuletea distributor wa hapo

Asante kwa ushauri Mkuu. Ila nadhani hata wao walipaswa kunitajia huyo distributors wao kwa ama pale Dodoma au pengine hata Dar-es-Salaam. Maana hata kama hawauzi nadhani basi walipaswa kunipa majibu haya ulonipa wewe.

Asante Kiongozi!
 
Ingia kwenye website yao click distributors hapo utaletewa ramani ya tz then click mkoa uliopo watakuletea distributor wa hapo
Najaribu kupiga namba zao walizoweka bila ya mafanikio, naambiwa na vodacom kuwa "namba hizo zimebadilishwa"

Anyway i will keep on trying!
 
Hawauzi kwa mteja mmojammoja,nenda kwa distributors wao,hata kama ukijua price sio utakayouziwa hiyo ni price ya distributors.

Tangu lini mkuu? mie nilinunua pale moja kwa moja. Ni miaka kama 5 hivi iliyopita.
 
Mkuu wewe ni mteja wa reja reja au wa jumla? Wale mara nyingi wanauza kwa wateja wa wholesale. Kama mahitaji yako hayajai kibaba, neda kwa wasambazaji wao... Pole...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…