mlonge oleifera
Member
- Jun 6, 2017
- 19
- 8
Mimi ni mjasiriamali ,ni mwenyeshule iliyosajiliwa .Nilikua natoa darasa la saba la Mara ya pili kisanga cha kuundiwa kesi ya uhamiaji kikanifika Mungu bariki nilijitetea na kupewa haki yangu ya uzawa.Pamoja na hayo nilikuta kati ya wanafunzi 200 nimebakiwa na 30 kwa hofu kuwa serikali itafunga shule hii na kuifilisi.Nilikua na mkopo , pia nikawa na miaka miwili ya hasara sasa nimezidiwa pamoja na kua sasa nimepambana na Nina wanafunzi 130 ,eneo la shule ekari 7 mjini, magari mawili ( hiaces) na watumishi 11. Ombi langu ambaye anamjua muhitaji ubia aje +255767928167 au +255621041167 pia wenye ushauri munipe namna ya kuziba mashimo haya ya madeni na kurudi musitarini.