Natafuta mbia pamoja na ushauri

Natafuta mbia pamoja na ushauri

Joined
Jun 6, 2017
Posts
19
Reaction score
8
Mimi ni mjasiriamali ,ni mwenyeshule iliyosajiliwa .Nilikua natoa darasa la saba la Mara ya pili kisanga cha kuundiwa kesi ya uhamiaji kikanifika Mungu bariki nilijitetea na kupewa haki yangu ya uzawa.Pamoja na hayo nilikuta kati ya wanafunzi 200 nimebakiwa na 30 kwa hofu kuwa serikali itafunga shule hii na kuifilisi.Nilikua na mkopo , pia nikawa na miaka miwili ya hasara sasa nimezidiwa pamoja na kua sasa nimepambana na Nina wanafunzi 130 ,eneo la shule ekari 7 mjini, magari mawili ( hiaces) na watumishi 11. Ombi langu ambaye anamjua muhitaji ubia aje +255767928167 au +255621041167 pia wenye ushauri munipe namna ya kuziba mashimo haya ya madeni na kurudi musitarini.
 
Pole mkuu.. Shule ipo mkoa gani? Umeongea na benki/mkopeshaji kuona kama anaweza ku-reschedule muda wa kulipa huo mkopo ili upumue kidogo?
 
Nlifkir unataka kuifufua namfua aisee ile ya rombo
 
Mkuu, nilifikiri uko karibu kumbe ni Manyara. Mi niko Dar.

Kama mkopeshaji wako hasomeki, na kama unayo business plan ambayo ni convincing, waweza jaribu kuona wakopeshaji wengine, unaweza pata atakayekubaliana na ww, anunue hilo deni, halafu mkubaliane utaratibu wa ulipaji unaokupa unafuu.

Option nyingine inaweza kuwa kutafuta mmiliki mwenye shule kubwa nzuri hata mkoa mwingine mwenye nia ya kufungua tawi la shule huko north, ukaingia naye ubia, au umuuzie (kwa kiwango cha kukuwezesha ku settle hilo deni na kupata chochote) then ujipange upya.. nk
 
Nashukuru wadau kwa ushauri wengine kwa kupitia manake ulivutiwa hatakama hukushauri waweza kumuelezea ambaye hayuko hapa jf mwishowe nikapata suluhisho la Baraka na haraka
 
Back
Top Bottom