Natafuta Mbuzi bora wa Nyama Madume aina ya Savanna na Boar hapa Tanzania

Natafuta Mbuzi bora wa Nyama Madume aina ya Savanna na Boar hapa Tanzania

Bugota

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
265
Reaction score
145
Wana Jamvi salama jamani.
Karibuni katika jukwaa let us la kilimo na mifugo.
Mimi ni mmoja wa wafugaji wadogo magharibi mwa Tanzania ninafuga ng'ombe na mbuzi wa kienyeji.
Nina hitaji la kuboresha mbegu ya mbuzi wangu ili kupata mbegu bora ya mbuzi wa nyama wanaokua kwa haraka zaidi.
Nina shida na mbegu ya madume wafuatao kama wapo hapa Tanzania:
1. Savanna
2. Boar
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho ya mjasiliamali mmoja aliyepo Uganda anaitwa HAMIISI SEMANDA ambapo amekuwa akionyesha kuwa mbegu hizi za mbuzi aina ya Savanna na Boar ni nzuri sana na tayari wao kule Uganda wameenda mbali hadi level ya Ranchi kubwa za maelfu ya mbuzi..
Sijui ka
 
Mkuu ukitaka taarifa za uhakika ni vizuri ukawasiliana na wizara ya ufugaji pale wana list ya ranchi zote tanzania na aina ya mifugo. itakuwia rahisi kupata ranchi yenye breed halisi unayoitaka. wengine huku magumashi, unapotaka kuchagua mbegu ni vizuri uwe makini kuepuka janjajanja.
 
Asante sana Ndugu yangu kwa kunishauri vizuri. Nitatafuta mawasiliano yao ila sema Taasisi zetu huku Tanzania zimelala.
Yaani hata hawajitangazi sijui wanataka nini.

Hawa ndugu zetu waganda wametupiga bao. Mfuatilie huyu jamaa Hamiisi Semanda kwenye youtube utapata kitu.
 
Magharibi ipi mi ndo nimemaliza mabanda Ngara. Wilaya ya Longido nimewaona mbuzi wazuri weupe breed ya Kenya nimesahau jina, ni Wakubwa kama hizo breed ulizotaja ila hawana complications, ni kama local breed. Sasa kuwafikisha magharibi ndo sijui.
 
Mkuu mimi niko nafugia Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kibondo karibu kabisa na Mto Malagarasi.
Tuna share same interest ni PM tuongee mengi na kwa sababu mimi makazi yangu ni Kahama mkoani Shinyanga ni rahisi tukajiunga tukachangia usafiri tukaenda kuwaleta hawa mbuzi kutoka huko Arusha.
 
Hao Mbuzi weupe ndio Savanna Mkuu. Halafu Boer wenyewe huwa weupe lakini huku kichwani na shingoni ni lazima wawe wekundu ndio tofauti ya hawa mbuzi. Lakini sifa zingine wanafanana na ndio mbegu bora kwa ajili ya ufugaji biashara maana wanakua haraka zaidi.
 
huyu jamaa yuko moshi rombo anao 0766499336
 
Mkuu mimi niko nafugia Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kibondo karibu kabisa na Mto Malagarasi.
Tuna share same interest ni PM tuongee mengi na kwa sababu mimi makazi yangu ni Kahama mkoani Shinyanga ni rahisi tukajiunga tukachangia usafiri tukaenda kuwaleta hawa mbuzi kutoka huko Arusha.
Kuna kijana anatafuta ajira ya umeneja wa ranch (shamba la mifugo) pamoja na kuwatibu, amesoma animal health and production.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahama na Kibondo? Unawasimamiaje. Kuwasimamia ukiwa mbali ni changanoto kweli kweli. Unafanyaje.
Nilikuwa nao 200 Vigwaza, mie naishi Dar. Huo mchakamchaka mpaka nikawauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu hebu tupe changamoto kubwa ilikuwa ni nini hasa? Mim nategemea kuanza ufugaji wa mbuzi na Ng'ombe wa nyama hvi karibuni. Nongependa kujua changamoto kubwa ilikuwa ni nini hasa
Kahama na Kibondo? Unawasimamiaje. Kuwasimamia ukiwa mbali ni changanoto kweli kweli. Unafanyaje.
Nilikuwa nao 200 Vigwaza, mie naishi Dar. Huo mchakamchaka mpaka nikawauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUO
 
Kuna kijana anatafuta ajira ya umeneja wa ranch (shamba la mifugo) pamoja na kuwatibu, amesoma animal health and production.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi sijafikia katika level ya Ranchi bali mfugaji mdogo kabisa. Huwa napeleka Dakitari kutoka Shinyanga anaenda shamba kuangalia, kutibu wanyama na kufundisha vijana wangu akiwemo na mwanangu na sipati shida kabisaa.
 
Ukiwapata ulete mrejesho ila angalia wajanja

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kahama na Kibondo? Unawasimamiaje. Kuwasimamia ukiwa mbali ni changanoto kweli kweli. Unafanyaje.
Nilikuwa nao 200 Vigwaza, mie naishi Dar. Huo mchakamchaka mpaka nikawauza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nakaaa Kahama kwa sababu bado ni mwajiriwa na nimeona siwezi kusubir kazi iishe ndipo nianze kuandaa mashamba/Mifugo na hapa ndipo watumishi wengi tunaharibikiwa. Anza kazi za ujasiliamali ukiwa bado uko kazini ili uiboost miradi ukiwa na nguvu isimimame then ikitokea umepoteza kazi basi angalau miradi yako itakuwa imeanza kuzalisha vitu kadhaa kama ulisimamia sawa sawa.
 
Ukiwapata ulete mrejesho ila angalia wajanja

Sent from my iPhone using Tapatalk
Moshi nina mfanyakazi wenzangu huku Kahama then nitasubiri akienda likizo nimpe nauli aende kuthibitisha kama wapo na tutaanzia hapo.
 
Moshi nina mfanyakazi wenzangu huku Kahama then nitasubiri akienda likizo nimpe nauli aende kuthibitisha kama wapo na tutaanzia hapo.

Bora
Good luck

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Habari wana jamvi. Nimempigia simu huyu ndugu wa Rombo kasdema hafugi mbuzi bali kuku tu hivyo bado naendelea kufuta hawa mbuzi ( Savanna and Boer)
Tuwasiliane mzee na mimi natafuta hao mbuzi
 
Mbeya wapi
Mkuu mimi niko nafugia Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kibondo karibu kabisa na Mto Malagarasi.
Tuna share same interest ni PM tuongee mengi na kwa sababu mimi makazi yangu ni Kahama mkoani Shinyanga ni rahisi tukajiunga tukachangia usafiri tukaenda kuwaleta hawa mbuzi kutoka huko Arusha.
Mbeya wapo,hata nanenane mbeya huletwa
 
Mbeya wapi

Mbeya wapo,hata nanenane mbeya huletwa
Nipe mawasiliano na kama unawajua fika basi nielekeze ni wilaya gani na sehemu gani ili nitume watu wangu wa karibu walioko Mbeya wakathibitishe
 
Back
Top Bottom