Northern Lights
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 395
- 357
Mkuu habari za leo, unaendeleaje na shughuli za ufugaji?Nikweli unacho kisema lakini hao wanao zaa mapacha ni wali Cross walipo kuja kenya, asili kabisa ya hawa Isiolo ni kuzaa mmoja, na nakubaliana na wewe kabisa waliingizwa Kenya kwanza kabisa ktk kaunti ya Isiolo.
Ni kweli ukuwaji wao ni wa haraka na wana jaza nyama vyema ktk miili yao.
Na niwavumilivu sana ktk hali ya hewa hasa hiki kipindi cha ukame,
Na niwavumilivu sana kwa magonjwa ila wakipata ile homa ya mapafu hawapindui.
Nina ushaidi ktk shamba langu nilipatwa na mkasa wa GOAT POX ugonjwa huu uliua Mbuzi wengi sana shambani kwangu lakini jamii ya ISIOLO/GALLA hawakudhurika na huo ugonjwa.
Nilikuwa na Mbuzi 168 nimebakiwa na Mbuzi 15 kwa sasa,
Chanjo na tiba ni vitu muhimu sana ktk ufugaji wa Mbuzi, na quarantine pindi unapo ingiza mfugo mpya ktk zizi lako.
Kwa sasa una breed gani shambani kwako na je uko mkoa gani? Ningependa kujifunza zaidi kuhusu ufugaji. hasa wa mbuzi