Natafuta mchumba muathirika

Natafuta mchumba muathirika

Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

Sitaki hata kujua jinsia yako, ila nakushauri kapige kikombe kwa babu kwanza, ikishindikana ndo urudi kutafuta na ukumbuke kuweka jinsia yako. Pole sana mungu akupe uzima.
 
Popote ulipo nenda ktk hospital uliza ward za waathirika/wenye ukimwi watakuonyesha jichagulie mwenyewe! Au nenda tume ya kudhibiti ukimwi watakusaidia kumpata mwandani wako!

Unyanyapaa huo
 
Popote ulipo nenda ktk hospital uliza ward za waathirika/wenye ukimwi watakuonyesha jichagulie mwenyewe! Au nenda tume ya kudhibiti ukimwi watakusaidia kumpata mwandani wako!

Haya na we ulipokurupukia, amekwambia ana ukimwi, au kuathirika ni ukimwi tu? Kidole kimoja kwa mwenzako, vitatu kwako.
 
nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.
hakikisha umepima mara 3 na mwenzio hivyohivyo.
 
Nimegundulika nina virusi vya Ukimwi baada ya kwenda kupima kwa hiyari, sina tatizo lingine la kiafya pia nina cd4 za kutosha hivyo sijaanza kutumia dozi.

Pole sana mpendwa, ila si lazima alieathirika hata mzima mkikubaliana mwaweza ishi bila maambukizi yeyote. Mtegemee sana mungu wako kwani mungu wetu ni mungu wa yasiyowezekana.
 
Hukutaja jinsia yako lakini nakushauri tulia muombe mungu atakupatia mwenza wako wa maisha, kuathirika sio mwisho wa yote maisha bado yanaendelea.
 
Popote ulipo nenda ktk hospital uliza ward za waathirika/wenye ukimwi watakuonyesha jichagulie mwenyewe! Au nenda tume ya kudhibiti ukimwi watakusaidia kumpata mwandani wako!
Hv huko ghorofani kuna kitu kweli jamani?
 
Wa mabomu ya gongolamboto ha haa haaaa!

mwenzetu ana shida mzaha si mahali pake, (una umri gani pengine utoto unakusumbua!) pole ndugu yangu mwaya maadam hii forum wengi wana i-view utafanikiwa na mungu akutangulie ktk hili
 
Mungu atuepushe wandugu. Leo nimeenda pale Bugando hosptl kwa macho yangu nimewaona waathhrika wenzetu wa magonjwa mbalmbal ikwemo HIV, kisukal,etc. Ila kuna wengine wanatumia hzo arv wana afya njema, wamenenepa vilivyo wengine wapo hoi, others wamepandwa na kichaa. Wakati napeleka specimen zangu stul na urine pale labaratory nkakuta dada mmoja bonge jeupee wa pale crdb nyanza branch anapima cd4, nikajiulza je kama huna vvu unaweza pima cd4?
Tujiulize nafc zetu sisi ni wazma, tena bila kunyosheana vidole.!
BACK TO U KAKA: nakushauri achana kabisa na swala la mchumba kwa sasa utadhoofka sana, jiangalie afya yako tu.
penda mambo kama, kula mlo kamili, mazoezi sana, kusali sana, kucheza na kuangalia mpira, kuangalia sinema, kusoma vtabu, fuata ushauri wa daktari na uishi kwa matumaini.
acha kufikiria sana una ukimwi kwani mawazo ndiyo yanaua waathrka wengi.
 
puuuuu nimependa ushauri wko wa kutokunyosheana vidole. Ila wa kwa huyo kaka mmmh kutafuta mwenza,mwandani wake ni muhimu mno why: watakua wanatiana moyo wa kujichukulia hali zao kama walivyo ili kurefusha siku ya kuishi pia upweke ni donda ndugu dear yaani kama jamii imemnyanyapaa!? No. Imeandikwa SI VEMA MTU HUYU AWE PEKE YAKE BALI NITAMTAFUTIA MWENZA WA KUFANANA NAYE! ingawa nikweli sala,mazoezi,lishe bora ni muhmu na huyo mwenza ndo atakayemtia moyo. USHAURI; tafuta ambaye si pasua kichwa akadhofisha afya yako
 
Bado unayo nafac ndugu yangu.! Mkabidhi mungu maisha yako, kuwa mvumilivu.
 
Lakini nina swali kwa wewe mtafutaji wa mchumba mwathirika.

1. ulijuaje mchumba wako wa kwanza hajaathirika??? Je mlienda kupima pamoja au..?
kwani umedai yeye hajui wewe ni mwathirika na alikuwa tayari kufanya tendo la ndoa na wewe................ UNA UHAKIKA GANI KUWA YEYE SIO MWATHIRIKA KAMA HUJAENDA KUPIMA NAYE???

baada ya kupata jibu lako ndio nitakupa POLE yangu - otherwise nina mashaka kuwa usemalo ni kweli .......... SAMAHANI LAKINI... KWA SWALI LANGU

AULIZAYE ATAKA KUJUA.....:argue:
 
Nashukuru kwa swali lako zuri, kuhusu mchumba wangu wa kwanza tumeshawahi kupima pamoja zaidi ya mara moja. Huyu wa pili sina uhakika sana lakini amewahi kutoa damu kwa mgonjwa mara mbili mwenyewe nikishuhudia na damu ilitolewa baada ya kupimwa sasa hapa sina uhakika sana kama hata waathirika hutolewa damu.
 
Nina umri wa miaka 35 natafuta mchumba ambaye ni muathirika. Mimi mwenyewe ni muathirika nimegundulika mwaka huu mwezi Feb. Kazi yangu ni mfanyabiashara.

kwanza kabisa nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuliandika hili jamvini na kuwa wazi kwa lile unalotaka.ila umesahau kutaja jinsia yako lakini nahisi kama u mwanaume.
mimi binafsi pamoja na kuwa ni mpimaji mzuri wa afya yangu na kutokuathirika hadi sasa,sijawahi kuona kama virusi ni tatizo kwenye mapenzi ya dhati kwa waloridhiana kiundani.
nimesikitika kuona kuwa unajinyanyapaa mwenyewe kwa kudhani kwamba huwez pendwa na mtu asiyeathirika.
kama ningekuwa nakufahamu na kuwa na uhakika ya kwamba unavigezo nivitakavyo kwa mume nimkusudiaye,nakiri ningependa tukusudie katika hili na naamini tungetoa elimu kwa wengi.
mapenzi ya kweli hayajali afya,maumbile wala mazingira.uzima na kifo huja wakati wowote.
unaweza kuniPM kama utapenda kulijadili hili zaidi (na niko serious)
 
Nimeipenda sana hii firsty lady, nakupenda hata wewe mwenyewe nakupenda sana. Kuna watu kama 25 hivi humu JF nawapenda sana miongoni mwao ni Wewe, Mzizimkavu, Michelle, Sizinga, Ivuga, Anfaal, 3D, GAZETI, Bubu ataka kusema, mzee mwanakijiji, susy, Denaamsi, Baba desi, Husniyo, sweetlady, Firstylady1 n.k huwa nafurahia sana baadhi ya michango yenu. Mwisho naomba unipe ufafanuzi wa signature yako hapo chini sijaielewa vizuri!
 
Back
Top Bottom