Kwanza nakupongeza kwa kujitambua na kuwa muwazi, Mungu akupe moyo wa kijasiri zaidi.
Pili ningependa kufahamu unamaanisha nini unaposema mwanaume aliye na hali kama yako? je, unamaanisha awe HIV+ pia?
Mimi ninakushauri utafute mwanaume yeyote aliye tayari, si lazima awe HIV+. Nasema hivi kwa sababu wengi wenye hali hii ni wazito kufikiria mbele kama wewe. Wengi hawapati ushauri nasaa na tiba ya kisaikolijia kujikubali kama ulivyojikubali wewe. Wengi wameshakata tamaa!
Ondoa hicho kigezo cha HIV+, werevu wataelewa na watakuja.