Natafuta mdhamini kwa mkataba maalum

Wanajukwaa na wasalimu kwa jina la Jamhuri Tanzania.

Ndugu zangu kiukweli nahitaji mtu ama Taasisi yeyote ya kuweza kunisaidi kumalizia miradi yangu ambayo nimekwisha ianza.


Karibu singid.
Haya makosa yalini gharimu kuwa makini sana unapofanya investment uwe tayari una uhakika wa kukamilisha vinginevyo hata ulichokianzisha kitaharibika bure
 
Punguza tamaa, inaonekana unatamaa ujamaliza hiki unakimbilia hiki kwa haraka haraka hata ukipata mbia kakupa pesa utenda anzisha jambo jipya,

Ushauri wangu uza miradi mitatu kamilisha miwili
Inawezekana siyo inshu ya tamaa ila alikuwa analamba asali,mirija imekata ghafla huku miradi mingi aliyoianzisha kwa pamoja ndiyo Kama hivyo haijaisha. Katika Hali ya kawaida mtu hwezi kuanzisha miradi mingi hivi alafu ikakwama kwa pamoja.

Nawaza tu,no hate.
 
Punguza tamaa, inaonekana unatamaa ujamaliza hiki unakimbilia hiki kwa haraka haraka hata ukipata mbia kakupa pesa utenda anzisha jambo jipya,

Ushauri wangu uza miradi mitatu kamilisha miwili
Mkuu naomba nieeleze jambo moja ala kama utabaki na msimami wako huu basi nitaendelea kueshmu mawazo yako mkuu.

Kwanza naomba ieleweke nilikuwa ninamtaji mkubwa wa matofali kwa sababu nilikuwa nafyatua mwenyewe,pia ninashimo la mchanga pia ninauza cement na matofali. Kwa kipindi hicho
Kwahiyo ujenzi si shida ilikuwa,ndiyo maana umeona nimeweza kujenga ila finishing ndiyo nimeshindwa na wala sikutegemea kushindwa ila kutokana na changamoto kwa sasa niliyonayo.

Kwahiyo faida yangu niliyokuwa napata napeleka kwenye ujenzi na kuendesha familia. kwa hiyo nilitumia fursa ya kupata raw materials ya ujenzi kwa ulaisi niliweza kumaliza kujenga. Binafsi nilihitaji kumaliza ndoto zangu kwa kutumia kitu nilichokuwa nacho kwa muda huo sikutaka kusubiri hadi nipate kitu ambacho sikuwa nacho kwa muda huo.

Kwa vile ninaliona ninamtaji mkubwa wa tofali nikaona niyatumie kukamilisha miradi yangu niliyonayo ili kulinda ardhi ala mambo mengine taratibu taratibu kwanza.

Kama nilikosea basi nahisi pasipo kujua kipi ni kipi kwanza kutokana na uelewa wangu. Asante
 
Salute kwako ....nenda NBC watakusaidiaaa.....chagua mradi mmoja au miwiliambayo itazungusha pesa .....mfano machine kusaga na kuamua alizeti....hilo naenda mpira pambana uezeke kabla August....league zote zitaanza tena .....utapata hela zako badilisha ziweke bank mzunguko uonekane....I'll ukopesheke
 
Nashukuru kwa ushauri mkuu,ukweli nilikwisha wai kukopa kiukweli nilipata shida nasa kwenye marejesho. Nilipo maliza nikajikuta nikauza mashine yangu ya tofali pia nikauza shimo langu la mchanga ili kumaliza marejesho.

Ila kuna mdau hapa amesema kuna bank inahitwa maendeleo sijajua wao wanautaratibu gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…