Natafuta mdhamini kwa mkataba maalum

Natafuta mdhamini kwa mkataba maalum

Emmanuel Mkwama

Senior Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
166
Reaction score
124
Wanajukwaa na wasalimu kwa jina la Jamhuri Tanzania.

Ndugu zangu kiukweli nahitaji mtu ama Taasisi yeyote ya kuweza kunisaidi kumalizia miradi yangu ambayo nimekwisha ianza.

1) Mradi wa kwanza kumalizia apartment mbili ambazo bado plaster, wiring ya umeme,madirisha ya vioo na mirango ya ndani.

2) Mradi mwingine ni wa ukumbi wa kuangalia mipira ambao bado kufunika,kupiga plaster pamoja na kusakafia. Ambao unao uwezo wa kuingiza watu 100 hadi 150. madirisha na mirango ipo tayari na nimekwisha ipachika.

3) Mradi mwingine ni wa kufunga mashine mbili wa kusaga nafaka pamoja na kinu chake cha kukobolea, na mashine nyingine ni mashine ya kukamua alizeti ili kutoa mafuta na kuyauza. eneo lipo tayari na jeongo lipo tayari kobado kumalizia ujenzi na kulitanua ili kupata sehemu ya kuhifadhia magunia ya alizeti na mashudu ambalo linahitaji kuongezea ujenzi. Pia kuna na ekari 25 kwa ajiri ya kupata raw materials ya kiwanda.

4) Kumalizia ujenzi wa nyumba ambayo nilifungua ili kuifanya kuw shule ya watoto wadogo kindergarten class ambayo bado kuifunika lakini ina vyumba vinne pamoja ofisi ya walimu kijiko pamoja na ofisi ya mwalimu mkuu ama Mkurugenzi. imebaki kuifunika na kuweka milango na madirisha pamoja na kuchimba shimo la choo pamoja na vyumba vya choo. hapo pana chemchem ya maji kwahiyo maji si shida

5) Mradi mwingine ni wa ujenzi wa mabwawa ya samaki eneo lipo tayari pana ekari 5 pia pana source ya maji ya chini nilikwisha anza kuyatafuta maji ya chini lakini si kumalizia nilipata shida binafsi.

6) Pia kuna frame za maduka inahitaji marekebisho kidogo ili watu waingine na biashara iendelee.

Kama kuna mtu ambaye anaweza kunishika mkoo tafadhali namuhitaji sana ambaye yupo seriously .
MAWASILIANO YANGU 0710468496
0717568496
EMAIL. emkwama@gmail.com
Karibu singid.
 
Punguza tamaa, inaonekana unatamaa ujamaliza hiki unakimbilia hiki kwa haraka haraka hata ukipata mbia kakupa pesa utenda anzisha jambo jipya,

Ushauri wangu uza miradi mitatu kamilisha miwili
Nimeona hivyo hivyo. Ukianza mradi mmoja umalize ndipo uanze mwingine. Uza umalizie mingine otherwise utatujazia magofu nchini
 
Punguza tamaa, inaonekana unatamaa ujamaliza hiki unakimbilia hiki kwa haraka haraka hata ukipata mbia kakupa pesa utenda anzisha jambo jipya,

Ushauri wangu uza miradi mitatu kamilisha miwili
Sio tamaa, jamaa ni mpambanaji sema tu kanuni ya "FOCUS" hajaiapply, angefocus na kimoja kimoja angekuwa anaetoboa
 
Hukua na haja ya kufanya miradi yote kwa pamoja ungeanza na mmoja ukamaliza ukaanza operation then unafuata mwingine hapo nenda bank tuu utpata mkopo ila lazima uweke bond,
kama biashara moja ingekua tayari basi bond ingekua biashara...
Yote tisa hongeraa sana
 
Nimeona hivyo hivyo. Ukianza mradi mmoja umalize ndipo uanze mwingine. Uza umalizie mingine otherwise utatujazia magofu nchini
Huo huwa ni ugonjwa so ukikosa tiba ya ushauri unakuathiri sana Kama mwamba hapa sijui alipata mafao au alipiga pesa sehemu maana kw akili ya darasa la tatu B huwezi anzisha vitu kiholela hivyo otherwise mwamba ni dalali kaona hivyo vitu kamua kuja jukwaani tafuta mbia
 
Hongera kwa miradi,ingia benki na nyaraka zako ni wiki tu una mpunga wa kutosha humu watakudhihaki tu
Huu ushauri ogopa tena ogopa jichanganye uone Bora ubaki unangalia magofu yako una amani kwenye nafsi yako , wenzako Wana biashara kubwa nk Ila hawana furaha wanawaza marejesho tu wanakula vizuri ila hawasikii radha ya chakula wanalala pazuri ila hawana usingizi Sasa jichomeke uko bank utarudi hapa jamvini ukweli hausemwi kuwa BANK KUZURI KUKOPA ILA SI KWAKILA MFANYA BIASHARA
 
Back
Top Bottom