Natafuta mfadhili nitamlipa zawadi nzuri

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Msema kweli ni mpenzi wa mungu
Maisha ni magumu, mshahara hautoshi halafu ukitegemea mwanaume akupe hela hakupi kwanza anakudharau anakuona huna maana.

Nimefikiria kuanzisha biashara ya saluni ya wanawake lakini sina hela yoyote.
Mimi ni mfanyakazi wa kawaida kutokana na imani yangu siwezi kukopa maana mikopo yote ina riba na mikopo ya riba huwa hailipiki itakuwa tu nafanyia benk biashara.

Ninajua kuna watu wana roho nzuri humu kwahiyo naombeni yeyote mwenye kuguswa anisaidie mtaji kidogo wa kuanzisha biashara hii nipo vizuri najua italipa
Kinachotakiwa ni hela ya kodi ya nyumba mwaka
3,600,000 Tsh

Kununua vifaa vichache 2,000,000Tsh
Operesheni zingine zitajilipia

Kama mtu anataka pia kuwa business partner ila awe na million tano anakaribishwa.
Kutakuwepo na chain ya biashara nyingi tu ila tunaanzia hapo
Asanteni
Nipo dsm
 
Be specific, Uko wapi na hyo biashara wawaza kuifanya mkoa gani au eneo lipi ndani ya nchi
 
Nenda benki ya Waislam mikopo haina riba
 
Jina lako Natafuta .... harafu umeandika "Natafuta" mfadhili.... ni coincidence tu au ndo mambo ya mjini suku hizi..... kama ni Genuine ishu... hongera kwa wazo la kuongeza kipato....
 
Nimefungua huu uzi fasta nikijua umeitaja hiyo zawadi nzuri...[emoji39] [emoji39]
 
Wewe una kiasi gani mkononi?
Utalipaje? Na kwa muda gani?
Dhamana itakuwa nini?
Eneo gani la Dsm?
Ulisha pata eneo la kupanga hiyo flem au bado ndoto?
Kama ni mfanyakazi umejipangaje kufanya hiyo kazi?
???????? Maswali bado mengi sana?
 
Miss natafuta katika utafutaji..., nimekuja nduki kudeku zawadi nzuri nakuta tarakimu za mijihela tu...
Wazo lako zuri kila lakheri
 
Tumia vitega uchumi vilivyokuzunguka kupata mtaji bibie...
 
upo tiyari kuzaa nae..kweli cipo kiutani..bro angu anasema anataka kuoa mwanamke ambae anajua kuhangaika kutafuta hela kupitia ujasiria malili..yeye yupo serikalini..hivo mda hana na anaamini kazi za kuajiriwa zina mwisho
 
Mkuu Miss Natafuta,umeshafanya utafiti walau kidogo juu ya ukubwa wa soko na eneo lako unapotaka kuweka biashara?
Umeshawahi kuifanya hiyo biashara au una uzoefu wowote wa biashara yoyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…