Natafuta mke asiyezidi miaka 30, si lazima awe na kazi

Natafuta mke asiyezidi miaka 30, si lazima awe na kazi

Wake wanapatikana misibani, kwenye sherehe, shule, ibadani, kwenye kusafiri, kazini au mtaani. Kwani wewe unaishi sayari ya mars?
 
Habari ndugu zangu,

Kama kuna mwanamke ambaye yupo tayari kwa ndoa namkaribisha mimi ni kijana ambaye:

1. Nimeajiriwa kwenye taasisi kubwa mjini
2. Umri wangu 34
3. Rangi ni mweusi
4. Muislamu

Ili mafanikio yapatikane ni kuwa na mke bora ambaye atakuwa na sifa zifuatazo:
1. Awe Muislamu
2. Awe ana rangi
3. Miaka isizidi 30
4. Sio lazima awe na kazi

N.B KARIBU PM ila naomba ukija uje serious maana lengo ni moja tu ndoa kama hauna nia bora utulie ili wenye nia waje maana naamini humu kuna wanawake wenye nia ya dhati ya kuolewa.
It will end in tears
 
Hiyo no.1 toa...
Anataka mwanamke wa kiislam.
Muafrika hataki kumuoa binti wa kiafrika asiyefuata dini toka uarabuni.
Hivi vigezo,ndo huwa vinanichekeshaga.
Kuna mtu namfahamu(sitamuita rafiki kwa sababu ya ubaguzi wake). Ukiwa si muislam,hata maji ya kunywa kwake huwezi kupata.
Basi,kaoa mwanamke eti kisa muislam. Kazaa nae,sasa hivi ana wajukuu. Mke,kashindikana(kwa anavyodai jama). Alivoona mkubwa anampanda kichwani,kaamua kumuoa wa 2. Si dini inaruhusu?! Nadhani kazaa nae watoto wawili,nae kamgeuka,kajiunga chama pendwa cha KATAA NDOA.
Sasa hivi,nadhani yupo katika harakati za kuoa mwingine tena. Ila sasa,nae kigezo kikubwa ni uislam.
Sasa,unajiuliza,muislam asiejitambua,na mkristo anaejielewa,yupi bora? Si kwamba wakristo hawana matatizo,ila, nahisi watu wangefikilia utu kwanza kabla ya madhehebu yao.


Hizi comment sizikuti katika nyuzi za wale wasio waislam wanaotafuta wenzao. Akhy anataka mke Muislam na ninamuomba Allah ampe mke mwema MUISLAM.

Hayo manung'uniko yenu bakini nayo wenyewe.
 
Back
Top Bottom