Natafuta Mke halisi wa kuoa ALIYEOKOKA


una shida gani mkuu, vuta ngoma ile uepuke mikuki ya pesa zavocha uswahilini, sio mchezo

unafumba macho na kulumangia kiskauti, ukimpuliza mara tatu kijeshi anakuwa mpole hatatusumbua tena na miripuko yake kama mchawi
 
Baada ya kuandika hizo sifa zote na kumaliza, bado unahisi umeokoka??
Nilidhani yule mwokovu ni yule anaemtegemea Mwokozi wake na kushukuru kwa kila jambo!
Bali ungalimo unaishi kwa SHERIA ..............!
 
Nakushauri hudhuria ibada za makanisa ya wakovu, huko utapata mke mwema.
 
Free advice:kwnn ucngeweka limit kwny hayo yote huwez jua waweza pata ambae hajaokoka lkn akaokoka kupitia ww..
 
Ushapata?
Bishanga mchokozi! mwenzio kaweka tangazo jana mara leo unamuuliza kama ameshapata! Ingekuwa rahisi kiasi hicho si angekuwa amepata kabla ya kutangaza? Lol!
 
Last edited by a moderator:
Mbona requirements/ criteria zinaonesha unataka asiyekuwa mlokole!


mwanamayu, we kwa mtazamo wako umeona criteria zinamgusa asiyeokoka/
Nadhani you are wrong

kwa uhakika wapo walio okoka wenye sifa tajwa hapo juu tena na zaidi ya hizo

then keep waiting be patient mwenyewe atapatikana kabisaaaa
 
Mimi ni Muislamu safi, niliyeokoka, sifa zote ninazo lkn ni mlokole wa kiislamu!!!
Je ninakufaaa?? km ndiyo, twende kwa PM
.

heshimu imani za wengine mkuu, hakuna mlokole wa kiislam.
Uislam hauko hivyo.
Usifanye kejeli kwenye imani za wenzako.
 
all the best mkuu, natumai utafanikiwa.
Nashauri ungeruhusa hata mwana jf anaemfaham mtu mwenye sifa unazotaka akuunganishe nae.
 

Mtu yeyote aliyeokoka kiukweli kama si wa magirini hawezi kumtafuta mke kupitia mitandao. Imeandikwa mke mwema hutoka kwa Mungu, na mali na utajiri mtu hupewa na babaye!!! Sijui wewe mchungaji wako alikufundisha nini kuhusu mke mwema na namna ya kumpata!!! Pole sana!!
 
nakushauli nenda kajipange hasa ktk maombi na kutoa kwa wingi maana mke mwema na bora ni yule anayetoka kwa Mungu tafuta mke ampendaye MUNGU Mwenye sifa kama hizi

SIFA ZA MKE MWEMA


Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10 hadi 31 kimeelezea sifa mbalimbali za mke mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo kwa kuzichambua katika maeneo tofauti. 1. Imani Mithali 31:26, 29, 30 Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi 119;15 2. Ndoa Mithali 31:11-12, 23, 28 Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3 3. Malezi Mithali 31: 26, 28 Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea. Mithali 22:6 4. Huduma Mithali 31:12-15, 17, 20 Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu. 5. Mali Mithali 31:14, 16, 18 Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23 6. Nyumba Mithali 31:15, 20-22, 27 Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2

lakini kama unataka mke wa kukutesa maisha yako yote na ukose na furaha endelea kutafuta humu ndani na kungineko kama sitofahamu.bye bye
 
Mbona requirements/ criteria zinaonesha unataka asiyekuwa mlokole!

Usijadanganye! wokovu upo akhera tena baada ya kufuzu katika mizani kubwa ya Mema na Maovu. Mizani yako ya hapa duniani ikiegemea kwenye mema utapata wokovu wa kweli na utakuwa ni mmoja watakaokirimiwa kila mema. Kufa basi uwahi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…