natafuta-mke-wa-maisha-umri-miaka-25-28

natafuta-mke-wa-maisha-umri-miaka-25-28

gize

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
202
Reaction score
134
Heshima kwenu wana Jukwaa

Natumaini kwa uwezo wake Mungu wote hatujambo. Kama kuna mgonjwa basi Namuomba Mungu amponye ili tuendeleze ujenzi wa taifa letu.

Nami leo Najitokeza katika jukwaa hili kutafuta Mke wa maisha yangu (Nipo serious katika hili),

A; Sifa zangu

Umri: Miaka 30
Kazi: Ninafanya kazi na ninakipato cha kunitosheleza kabisa kumudu mahitaji muhimu
Elimu: Nina degree moja
Urefu: Ni mrefu kiasi (Setimita 180) na Mwembamba kiasi
Rangi: Ni mweusi kiasi
Dini; Mkristu
Watoto; Sina mtoto
Matumizi ya vileo: Situmii Pombe ya aina yoyote wala kuvuta sigara etc

B; Sifa za Mke ninayemtafuta
Umri: Miaka 25-28
Dini; Mkristu
Elimu: Kuanzia Diploma na kuendelea
Munekano: MWEMBAMBA na MREFU angalau kuanzia Sentimita 170 na kuendelea (Ni moja wapo ya kigezo muhimu sana kwangu), pia ukiwa na mvuto nitashukuru zaidi
Kabila: awe kati ya - Mnyambo, Mkerewe,Mbondei, Mmeru, Mmburu, Mnyaturu, Mdigo au Mnyamwezi.
Kuzaa: Awe ambaye hajawahi kuzaa
Kilevi: Asiwe anakunywa pombe ya aina yoyote wala kuvuta Sigara etc
Rangi: Awe mweusi kiasi/ maji ya kunde
Kazi: Kama unayo kazi tayari nitashukuru zaidi lakini hata kama hauna hakuna shida
TABIA: AWE NA TABIA NJEMA NA ALIYETAYARI KUPIMA VIRUS VYA UKIMWI, NA AMBAYE ANAPENDA KUFUNGA NDOA MWAKA 2014-2015.

Tafadhali kwa MELEZO MENGINE YA NDANI ZAIDI NA KUFAHAMIANA KWA wale TU wanaokidhi vigezo tajwa hapo juu tafadhali NITUMIE PM yako au tuwasiliane kwa E-mail; gizewise@yahoo.com, BILA SHAKA YOYOTE PM na E-mail zote zitajibiwa bila shida na kwa haraka.

Tafadhali kama hauna vigezo tajwa usijisumbuke kuni PM wala kunitumia e-mail.
Asanteni; Natumaini nimeeleweka.
 
Fursa hizoooooooo.......

Kila la kheri mkuu I hope utampata mwenye kukidhi vigezo vyako
 
tangazo lako limesomeka vema ila ni wasiwasi huenda usipate any application kwa hofu ya kukwepa kigezo cha "...... ALIYETAYARI KUPIMA VIRUS VYA UKIMWI..". hapo wengi watakimbia
 
Vp ishu ya kupimana Ubavu itahusika au mtakutana kwenye Ligi baada ya ufunguzi? Ndugu yangu ongezea sifa za Jinsia ya Mke unaehitaji maana Bahari ya mapenzi imechafuka,Mibwabwa bin Mipunga itavamia Hiyo 'fursa' ikidhani nao ni washika dau!
 
Umepangilia pwenti zako vizuri, nimependa...
Mungu akujalie upate haja ya moyo wako!
 
Natamani watu wote wanaotafuta wenzi wangekuwa na uwezo wa kuainisha mambo kama wewe...

Unaonekana unajielewa na unaelewa nini unachokitaka, ninaamini Mungu atakupa mwanamke sawasawa na uhitaji wako...

Kila la kheri kaka mkubwa....
 
Siku hizi bila diploma ama degree binti hawezi kuolewa daaaah

hapana mkuu, ni matazamo tu.. nivizuri kuwa na mtu angalau mnayeendana kiulewa wa baadhi ya mambo kuepusha migongano isiyo ya lazima
 
watu8,
shukrani sana mkuu..Ujenzi mwema wa Taifa.

Natamani watu wote wanaotafuta wenzi wangekuwa na uwezo wa kuainisha mambo kama wewe...

Unaonekana unajielewa na unaelewa nini unachokitaka, ninaamini Mungu atakupa mwanamke sawasawa na uhitaji wako...

Kila la kheri kaka mkubwa....
 
Duhh mkuu Songoro

Nimekupata, ila mengine ni ya ndani sana.. si vizuri kuyaweka hapa, ni kama nitakuwa nawakosea heshima.

Asante kwa angalizo

Vp ishu ya kupimana Ubavu itahusika au mtakutana kwenye Ligi baada ya ufunguzi? Ndugu yangu ongezea sifa za Jinsia ya Mke unaehitaji maana Bahari ya mapenzi imechafuka,Mibwabwa bin Mipunga itavamia Hiyo 'fursa' ikidhani nao ni washika dau!
 
epson
Ngoja niamini wapo ambao wako tayari kupima VIRUSI VYA UKIMWI,
Asante kwa tahadhari... Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Pamoja sana.

tangazo lako limesomeka vema ila ni wasiwasi huenda usipate any application kwa hofu ya kukwepa kigezo cha "...... ALIYETAYARI KUPIMA VIRUS VYA UKIMWI..". hapo wengi watakimbia
 
Sasa hivi umetulia hadi umeamua kuoa eeh,
Hivi unaona kabila au unaona mwanamke?
 
Mamndenyi
Mimi nimtulivu kwa asili, ila ndio hivyo tena utulivu wangu na kuwa mkweli ndio imekuwa changamoto yangu ya kutodumu na hawa wadada..
Naoa mwanamke ambaye ametokea katika mila na desturi za kabila fulani, zenye mtazamo na misimamo ya kabila hilo.
Asante.

Sasa hivi umetulia hadi umeamua kuoa eeh,
Hivi unaona kabila au unaona mwanamke?
 
Back
Top Bottom