Natafuta mke

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] anza na waliopo mtaanii..mnataka kula kimasikhara watoto wa watu nyinyi
Ukisoma vizuri, usingeniambia hili jambo!?

Mie natoka kwa buza huku,kwa mpalange hakuna watu hawa sasa [emoji23]
 
Nakutakia ushindi kwa haraka , ila ingekua na uzito ungeambatana na "Swalat-istighara" ili upate "mke halisia sio bora mke"
 
Tafuta mrembi hapo msikitini
Tumia akili kubwa futilia wadada watatu wanaoswali sana sana chunguza tabia ukishawafahamu tongoza mmoja au wawili thenunakuwa umepata mkr mkuu .Very simple tu Mkuu.
 
Sasa bila picha itakuwaje
Itakuwa hivyo hivyo tu chief..

Picha sio muhimu saana, hujafa hujaumbika, vipi kaja kwangu kanipendea sura yangu kesho na kesho kutwa nimepata ajali sura imeharibika, vipi akapenda rangi yangu, ikatokea imeharibika..
Kwanza utayari wa mtu kumpokea mtu katika mazingira yoyote..
Picha nimeweka namba ya simu atakaehitaji nitampasia huko chobingo.


Vipi chief unataka nikuwekee wewe.. (Joke) [emoji23]
 
Nakutakia ushindi kwa haraka , ila ingekua na uzito ungeambatana na "Swalat-istighara" ili upate "mke halisia sio bora mke"
Shukrani kwa ushauri chief..
Najitahidi kufanya hivyo, inshaallah mola mlezi ataleta kheri.
 
Tafuta mrembi hapo msikitini
Tumia akili kubwa futilia wadada watatu wanaoswali sana sana chunguza tabia ukishawafahamu tongoza mmoja au wawili thenunakuwa umepata mkr mkuu .Very simple tu Mkuu.
Ahsante kwa mawazo yako pia, nayo ni moja ya njia, ila si rahisi saana kwa msikitini nadhani unaelewa mazingira ya kuswali kwetu waislaam, si rahisi kumuona mtoto wa kike na pia wanawake weengi huswalia majumbani.

Nilichoweza kufanya ni kuwashirikisha maimam wa misikiti kadhaa kama atatokea mtu anahitaji stara, wa vigezo kadhaa basi wanifahamishe.
 
Naogopa siku uje kuniolea wake wengine 3 duh[emoji6] Moyo wangu ni mwepesi+wivu [emoji19]
Binafsi sijawahi kufikiria kuoa zaidi ya mke mmoja at STP[emoji23].

Labda kutokee sababu nje, ambayo inawezekana kuoa ikawa ni solution..
Kuoa mke zaidi si jambo la wepesi kuna uzito wake na unaweza jikuta unapata dhambi badala ya thawabu..

Sura an nisaa aya ya 3 kaelezea hilo jambo, ila tukianzia aya ya kwanza tunaweza faidika vizuri..

1. Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni

2. Na wapeni mayatima mali yao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika yote hayo ni jukumu kubwa

3. Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.
 
Hapana mkuu mimi nakufahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…