NATAFUTA MKE(MWANAMKE WA KUOA)
Assalaam aleykum warahmatulahi ndugu zangu
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza natafuta mke wa kuoa.
Mtu atajiuliza why, nitafute mtandaoni !? [emoji15]
Binafsi naamini waliokuwepo mtandaoni ni sawa na waliokuwepo mtaani, kuna watu safi, kuna watu waovu vike vile, kama ambavyo mtaani wapo, lakini mtandao unanikutanisha na watu ambao katika maisha yangu ya kila siku si rahisi kukutana nao.
Kwanini nataka kuoa
Kwanza ni sababu dini yangu imenitaka mimi nioe, ndoa ni utulivu wa nafsi, ndoa ni nusu ya dini, ndoa ni stara.
Binafsi naona ibada ya swala bila ya kuwa na ndoa nakuwa katika kucheza pata potea, na hili ndio linalonisukuma hasa hasa kutaka kuoa, ili nipate kufanya ibada vema, ibada zenye uzito mkubwa ndani yake..
Pili kuna maisha fulani natamani kuishi ila haya pasina mke bora(mcha mungu) sioni kama nitaweza kuishi walau robo yake.
Mwanamke wa aina gani !?
Kama naoa sababu dini, basi sina budi kuoa mwanamke ambae dini yangu imenifundisha(imenielekeza) kuoa.
Rasulillah s.a.w ametufundisha mwanamke anaolewa kwa mambo manne(4) i.e dini yake, nasaba yake, uzuri wake na mali yake, hivi ndio vigezo, katika hivi kila mtu atachagua kwa kigezo ama vigezo katika hivi vi4
binafsi nikiambiwa nichague kigezo kimoja tu, basi nitaoa mwanamke kwa dini(uchamungu) natafuta mwanamke tuishi hali ya kuwa duniani tunapita, tuishi kwa ajili ya kesho yetu, na inshaallah mola wetu akituridhia atutie katika pepo yake, nae akawe huraini wangu peponi.
Kwa mimi.
DINI- awe na elimu kubwa ama ndogo ya dini sijali, muhimu awe tayari kuishi kwa ajili ya kesho yetu
NASABA-kwa mtandaoni hiki kigezo nakosa hata cha kuzungumzia, ni kigezo muhimu saana, wazee wetu wa zamani hata kama dini walikuwa hawajui saana, ila walifaulu kwa kigezo cha nasaba, maana ukoo mwingine mtihani mtupu, unaweza ukauingia ukoo una maswahibu yake sio mchezo, walikuwa sahihi kuoeleana, makaveli mwanangu anataka kuoa naenda kumposea kwa mzee njukuru sababu naujua ukoo vizuri, wakati mwingine binti anakuwa namuona malezi ya bwana njukuru nayajua, yeye bwana njukuru ananijua vema, hii ndoa ikawa rahisi, lakini siku hizi tunaokotana okotana, na maisha yetu ya kimjini ndio mtihani..
Allah anifanyie wepesi katika hili, yeye ndio mjuzi zaidi anayajua yale yaliyodhahiri kwangu na yasiyokuwa dhahiri.
UZURI- uzuru wa mtu uko machoni kwa mtu, kwangu mwanamke akiwa mweupe, pua ndefu kidogo, kasura kazuri zuri kidogo(sura za kitusi) mrefu, umbo lolote kama, akiwa na vinyama nyama inapendeza zaidi.. Lakini akikosa kigezo chocjote hapa asijali, kwangu muhimu ni huo utayari wa kuishi kwa ajili ya kesho yetu, anaweza akawa na kigezo kimoja, au hana kabisa asijali.
MALI- kwangu awe nacho awe hana, hiki kigezo sikizingatii.
N.B sijata umri hapo, sababu mtume hakutaja umri, alioa wakubwa kwake na wadogo pia..
Kama atakuwa 30+ mpaka kwenye 40+ hivi itapendeza zaidi, ila hata km itakuwa chini ya hapo kweye 25+ si mbaya pia, awe mjane sijui nini, muhimu ni utayari wake kuishi maisha yanayompendeza mola wetu.
Mimi nani
Mimi ni kijana tu wa kiislaam, mweupe kiasi, mrefu, sina elimu kubwa saana ya dini, na pia nina elimu kiasi kwa elimu ya duniani, mwisho form 6, chuo nikasoma mwaka mmoja tu (....____) maisha yangu ni ya kawaida tu, alhamdulillah [emoji2972], vijana wa siku hizi wanasema nabangaiza.
Kipi nisichopenda.. 1. Kuacha kufanya ibada, 2. Usaliti. Hivi ndio vitu viwili vinaweza vikavunja na ndoa yenyewe, mengine tutavumiliana vumiliana, binadamu sie, si wakamilifu..
Moja ya sifa kuu ya ndoa ni kucover(kustiriana) pale kwenye mapungufu ya mwenzangu nimstiri nae kwenye mapungufu yangu anistiri
Ujana nimeufanya saana[emoji17] lakini nimekuwa nikiishi nakufikiria kesho yangu, najitahidi kufanya ibada kuna wakat najisahau, lakini kuna aina fulani ya maisha nayatamani na naamini pasina ndoa ngumu kuyaishi kwa kweli.
Kiukweli kabisa maisha ya dunia ni mpito tu.. Kesho yetu ni ndefu mnoo, maisha yake hayana mwisho, ikiwa nitamuelekea mola wangu hali kanikasirikia basi mimi ni mpotevu, na ikiwa nitamuendea hali hajanikasirikia basi nimefaulu, natamani niwe miongoni mwa wailofaulu.
Mtume Muhammad s.a.w
"Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora zaidi ni kumpata mke mwema."
Sambaza ujumbe huu kadri utakavyoweza uwafikie watu wengi wengi.
[emoji2972][emoji2972][emoji2972]
Allah atufanyie wepesi katika mazito yetu, atujaalie mema duniani na kesho akhera, atuepushe na moto, atuepushe na adhabu zake kali, atupunguzie uchungu wa umauti, atujaalie mwisho mwema, ajaalie makaburi yetu yawe viwanja katika viwanja vya peponi...
Wala tusiwe miongoni mwa waliopotea. Ya rabbi bila huruma yako sisi tumeangamia, bila ya uongozi(nusra) wako sisi ni wapotevu.
Nina mengi ya kuandika muda tatizo..
Wabillahi tawfiqi.