Natafuta mke

Natafuta mke

Mkuu vingine c unafanya kama unajikuna tu [emoji23] ...
Maaana kule jamaa alikuwa anaweza kuchambua tukio kwa picha tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Ujue Rebeca 83 namkosea jibu kamili [emoji23]

Fine yule ni mimi kweli, haimaanisha ndio sipaswi kuyajua, ujana nimeula ula saana, lakini sasa nimeamua dunia kuipa mgongo kweli, na naimani siwezi kumuabudu vizuri mola wangu pasina kuwa na utulivu wa nafsi, na utulivu wa nafsi ni kupata mke mwema kabisa, najijua, haya magumu ninayopitia kiboko yake ni kupata mke mwema..

Mtume Muhammad s.a.w "Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora zaidi ni kupata mke mwema"

Ili niipate starehe ya dunia iliyo bora zaidi lazima nipate mke mwema, nipate utulivu wa nafsi,
La sivyo ipo siku ibada zangu nitazitupa kama sukari ndani ya bahari.
 
Ujue Rebeca 83 namkosea jibu kamili [emoji23]

Fine yule ni mimi kweli, haimaanisha ndio sipaswi kuyajua, ujana nimeula ula saana, lakini sasa nimeamua dunia kuipa mgongo kweli, na naimani siwezi kumuabudu vizuri mola wangu pasina kuwa na utulivu wa nafsi, na utulivu wa nafsi ni kupata mke mwema kabisa, najijua, haya magumu ninayopitia kiboko yake ni kupata mke mwema..

Mtume Muhammad s.a.w "Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora zaidi ni kupata mke mwema"

Ili niipate starehe ya dunia iliyo bora zaidi lazima nipate mke mwema, nipate utulivu wa nafsi,
La sivyo ipo siku ibada zangu nitazitupa kama sukari ndani ya bahari.
inshaallah mkuu na sisi tunakufuata ,ila nikisikia neno ndoa sjui kwanini moyo unapasuka pa!
 
inshaallah mkuu na sisi tunakufuata ,ila nikisikia neno ndoa sjui kwanini moyo unapasuka pa!
Ni jambo zito kwa kweli, hasa ikitokea umetoa boko kwenye kuoa, utaona dunia ndio jehannam unayosikia, ila ukipatia mbona unajiona dunia umeumbiwa wewe pekee..

Kuna watu wana enjoy saana katka ndoa, kuna watu kwa ni tabu na karaha..

Kikubwa ni kuomba uongozo mzuri toka kwa mola katika jambo hili zito.
 
Itakuwa hivyo hivyo tu chief..

Picha sio muhimu saana, hujafa hujaumbika, vipi kaja kwangu kanipendea sura yangu kesho na kesho kutwa nimepata ajali sura imeharibika, vipi akapenda rangi yangu, ikatokea imeharibika..
Kwanza utayari wa mtu kumpokea mtu katika mazingira yoyote..
Picha nimeweka namba ya simu atakaehitaji nitampasia huko chobingo.


Vipi chief unataka nikuwekee wewe.. (Joke) [emoji23]
Nikiweka picha si itakuwa mvurugano mufti..

Mwishowe watajitokeza wengine hawana nia thabiti, wanafata muonekano wangu mbovu..[emoji1787]
 
Inanibidi na mie nivute jiko tu, huu ujana una mwisho wake ndugu yangu, maisha baada ya umauti ni marefu kichizi kuliko haya ya duniani, ukitafakuri vizuri utagundua vitu kadhaa
Kweli kaka umenena vuta jiko si tuliokwisha oa tutakuja kula ubwabwa
 
Tumetofautiana akili, kufikiri, maono n.k, so siwezi kukulamu kuhisi hivyo unavyohisi, huenda ndio akili yako ilipoishia..
Siwezi kukulazimisha uamini usichokiamink mzee
Haya ni maisha yangu binafsi, lau kama ungekuwa unamjua makaveli mwenyewe ungesadiki pasina chembe ya mashaka

Lakini pia unaweza kuwa sawa katika slogan hiyo, lakini tambua huwezi kuwa sawa nyakati zoote, maisha hayana formula kama kwenye physics na math's mzee..


Lakini yoote 9, 10 wewe sio muolewaji sheikh..(mnong'onezo)
Watoto wa mjini wanasema umempa za uso....
 
PM unayoizungumzia wewe private message, prime minister au post meridiem.. [emoji23]

...ha haha hahaha, ungeweza tu kusema hujaona PM yake au alimaanisha Poor Man

BTW, heri ya 2021 mdau na tembelea viwanja va Shababi uungane na maveteran wenzako wa Kigamboni
 
...ha haha hahaha, ungeweza tu kusema hujaona PM yake au alimaanisha Poor Man

BTW, heri ya 2021 mdau na tembelea viwanja va Shababi uungane na maveteran wenzako wa Kigamboni
Labda alimaanisha Power of Mundende..

Shukrani, heri iwe kwetu soote ndugu yangu, Nitasogea, kwanza najifua beach mkuu nipate mwendo kasi.
 
  • Thanks
Reactions: Obe
NATAFUTA MKE(MWANAMKE WA KUOA)

Assalaam aleykum warahmatulahi ndugu zangu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza natafuta mke wa kuoa.

Mtu atajiuliza why, nitafute mtandaoni !? [emoji15]
Binafsi naamini waliokuwepo mtandaoni ni sawa na waliokuwepo mtaani, kuna watu safi, kuna watu waovu vike vile, kama ambavyo mtaani wapo, lakini mtandao unanikutanisha na watu ambao katika maisha yangu ya kila siku si rahisi kukutana nao.

Kwanini nataka kuoa
Kwanza ni sababu dini yangu imenitaka mimi nioe, ndoa ni utulivu wa nafsi, ndoa ni nusu ya dini, ndoa ni stara.
Binafsi naona ibada ya swala bila ya kuwa na ndoa nakuwa katika kucheza pata potea, na hili ndio linalonisukuma hasa hasa kutaka kuoa, ili nipate kufanya ibada vema, ibada zenye uzito mkubwa ndani yake..
Pili kuna maisha fulani natamani kuishi ila haya pasina mke bora(mcha mungu) sioni kama nitaweza kuishi walau robo yake.

Mwanamke wa aina gani !?
Kama naoa sababu dini, basi sina budi kuoa mwanamke ambae dini yangu imenifundisha(imenielekeza) kuoa.
Rasulillah s.a.w ametufundisha mwanamke anaolewa kwa mambo manne(4) i.e dini yake, nasaba yake, uzuri wake na mali yake, hivi ndio vigezo, katika hivi kila mtu atachagua kwa kigezo ama vigezo katika hivi vi4
binafsi nikiambiwa nichague kigezo kimoja tu, basi nitaoa mwanamke kwa dini(uchamungu) natafuta mwanamke tuishi hali ya kuwa duniani tunapita, tuishi kwa ajili ya kesho yetu, na inshaallah mola wetu akituridhia atutie katika pepo yake, nae akawe huraini wangu peponi.
Kwa mimi.
DINI- awe na elimu kubwa ama ndogo ya dini sijali, muhimu awe tayari kuishi kwa ajili ya kesho yetu
NASABA-kwa mtandaoni hiki kigezo nakosa hata cha kuzungumzia, ni kigezo muhimu saana, wazee wetu wa zamani hata kama dini walikuwa hawajui saana, ila walifaulu kwa kigezo cha nasaba, maana ukoo mwingine mtihani mtupu, unaweza ukauingia ukoo una maswahibu yake sio mchezo, walikuwa sahihi kuoeleana, makaveli mwanangu anataka kuoa naenda kumposea kwa mzee njukuru sababu naujua ukoo vizuri, wakati mwingine binti anakuwa namuona malezi ya bwana njukuru nayajua, yeye bwana njukuru ananijua vema, hii ndoa ikawa rahisi, lakini siku hizi tunaokotana okotana, na maisha yetu ya kimjini ndio mtihani..
Allah anifanyie wepesi katika hili, yeye ndio mjuzi zaidi anayajua yale yaliyodhahiri kwangu na yasiyokuwa dhahiri.
UZURI- uzuru wa mtu uko machoni kwa mtu, kwangu mwanamke akiwa mweupe, pua ndefu kidogo, kasura kazuri zuri kidogo(sura za kitusi) mrefu, umbo lolote kama, akiwa na vinyama nyama inapendeza zaidi.. Lakini akikosa kigezo chocjote hapa asijali, kwangu muhimu ni huo utayari wa kuishi kwa ajili ya kesho yetu, anaweza akawa na kigezo kimoja, au hana kabisa asijali.
MALI- kwangu awe nacho awe hana, hiki kigezo sikizingatii.

N.B sijata umri hapo, sababu mtume hakutaja umri, alioa wakubwa kwake na wadogo pia..
Kama atakuwa 30+ mpaka kwenye 40+ hivi itapendeza zaidi, ila hata km itakuwa chini ya hapo kweye 25+ si mbaya pia, awe mjane sijui nini, muhimu ni utayari wake kuishi maisha yanayompendeza mola wetu.

Mimi nani
Mimi ni kijana tu wa kiislaam, mweupe kiasi, mrefu, sina elimu kubwa saana ya dini, na pia nina elimu kiasi kwa elimu ya duniani, mwisho form 6, chuo nikasoma mwaka mmoja tu (....____) maisha yangu ni ya kawaida tu, alhamdulillah [emoji2972], vijana wa siku hizi wanasema nabangaiza.
Kipi nisichopenda.. 1. Kuacha kufanya ibada, 2. Usaliti. Hivi ndio vitu viwili vinaweza vikavunja na ndoa yenyewe, mengine tutavumiliana vumiliana, binadamu sie, si wakamilifu..
Moja ya sifa kuu ya ndoa ni kucover(kustiriana) pale kwenye mapungufu ya mwenzangu nimstiri nae kwenye mapungufu yangu anistiri
Ujana nimeufanya saana[emoji17] lakini nimekuwa nikiishi nakufikiria kesho yangu, najitahidi kufanya ibada kuna wakat najisahau, lakini kuna aina fulani ya maisha nayatamani na naamini pasina ndoa ngumu kuyaishi kwa kweli.
Kiukweli kabisa maisha ya dunia ni mpito tu.. Kesho yetu ni ndefu mnoo, maisha yake hayana mwisho, ikiwa nitamuelekea mola wangu hali kanikasirikia basi mimi ni mpotevu, na ikiwa nitamuendea hali hajanikasirikia basi nimefaulu, natamani niwe miongoni mwa wailofaulu.
Mtume Muhammad s.a.w
"Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora zaidi ni kumpata mke mwema."


Sambaza ujumbe huu kadri utakavyoweza uwafikie watu wengi wengi.

[emoji2972][emoji2972][emoji2972]
Allah atufanyie wepesi katika mazito yetu, atujaalie mema duniani na kesho akhera, atuepushe na moto, atuepushe na adhabu zake kali, atupunguzie uchungu wa umauti, atujaalie mwisho mwema, ajaalie makaburi yetu yawe viwanja katika viwanja vya peponi...
Wala tusiwe miongoni mwa waliopotea. Ya rabbi bila huruma yako sisi tumeangamia, bila ya uongozi(nusra) wako sisi ni wapotevu.


Nina mengi ya kuandika muda tatizo..


Wabillahi tawfiqi.

You have always been my crush incase hukujua hili lol
Nasomaga tu comments natikisa kichwa
Mungu akujalie hili litimie[emoji1374]
 
Back
Top Bottom