Natafuta mkopo wa masharti nafuu

Natafuta mkopo wa masharti nafuu

kindili kindili

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
242
Reaction score
54
Katika mahangaiko ya maisha wandugu, nishapoteza laki 2 zinaniuma kinoma ila sijakataa tamaa naombeni mwenye kujua wapi ntapata mkopo wa masharti nafuu sana sina nyumba wala kiwanja wa kazi yangu ya muhindi haiwezi kunidhamini, any other way lakini pia nina akiba mil 2, je ninunue kijiasset kinachoweza nidhamini? kama kiasset kipi? majanga juu yake majanga, ninahitaji 5M

Wasalam, msakatonge na jua la dasilamu
 
mh!kama una hyo 2 ml c unaweza angalia biashara ya kufanya ukakuza mtaj kuliko majanga ya mkopo ?
 
Sikushauri kutumia hiyo 2 m kwa kununua kijiasset ili kiwe dhamana ya kupata mkopo wa m5. ni vema sana ikijipamga kuiwekeza hiyo m 2 katika mradi fulani.
 
Mkuu watu wanasaka laki tano ili watoke, sjajua una idea gani na hizo 5m unazotafuta, ungeweka wazi watu wangeweza kukushauri pengine kwa izo izo 2m ungeanza na kukuza mtaji wako. Halafu unaandika kwa kulalamika sana jikaze mkuu
 
wakuu nina idea na biashara lakini maeneo nayotaka kuiweka ni maendeo ya wakubwa kigd, nway nataka kufungua butcher, hy ndo biashara inayogonga kichwani kwangu, nimepiga mahesabu aina ya butcher nalotaka ili niweze kuteka soko 2m hazitoshi!!! kodi ya pango tu laki 7 na nusu, fridge laki 6, mzani na mzigo wa kuanzia na vikolokolo vingne...nina mshahara nategemea mkopo kulipa kupitia mshahara..so nachotaka ni kuivest mshahara wangu ujao kama nikiwa miezi ka sita hv
 
Sasa kijana kama una 2mill inatosha kuanzisha biashara pia mtu mwenye nia na biashara anaanza hata na mtaji wa laki 3 so tumia ulichonacho mkononi kuzalisha kisha tafuta kikundi cha watu 5 muenda FINCA mkachukue mkopo bila dhamana.
Katika mahangaiko ya maisha wandugu, nishapoteza laki 2 zinaniuma kinoma ila sijakataa tamaa naombeni mwenye kujua wapi ntapata mkopo wa masharti nafuu sana sina nyumba wala kiwanja wa kazi yangu ya muhindi haiwezi kunidhamini, any other way lakini pia nina akiba mil 2, je ninunue kijiasset kinachoweza nidhamini? kama kiasset kipi? majanga juu yake majanga, ninahitaji 5M

Wasalam, msakatonge na jua la dasilamu
 
Nunua boda boda uendeshe mwenyewe, kila siku hakikisha unasave kama 10 au zaidi kulingana na ulizopata. Ukitimiza hela ya kununua boda boda nyingine nunua na mkabodhi mtu halafu uwe unafatilia kwa makini as long as na wewe mwenyewe unaendesha sio shida.

Mtaji wa butcher utautimiza in 1.5 years, tena ni mil 7 sio tu 5.
 
Unaeza ukapata mkopo wenye mshart nafuu ila Riba ipo juu,sasa sijui lipi bora,ila ni vema ukawa ckiiza wadau wanasemaje hapo juu
 
ndio mkuu godi mpare, nimefanya reserch ya kutosha na faida ipo
 
kudunduliza ndugu yangu ndio mkopo pekee wenye riba nafuu (kujibana kimatumizi). Mikopo mingine yote ni photocopy
 
Back
Top Bottom