Natafuta mshirika katika ufugaji wa kuku wa kienyeji

Natafuta mshirika katika ufugaji wa kuku wa kienyeji

Jogoo10

Senior Member
Joined
Jul 22, 2014
Posts
100
Reaction score
11
Namini msemo usemao kidole kimoja hakivunji chawa. Na umoja ni nguvu. Mm ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, nina ujuzi na uzoefu wa eneo hili. Nipo nje kidogo ya dar kilwa road. Tayari nimesha andaa mabanda ya kutosha, fens ni ufugaji nusu huria tayari nimeweka makoo na majogoo na vifaa vyote, kopo za vyakula za kutosha na kopo za maji. Kuku washaanza kutaga vifaranga 100 kila baada ya wiki 3 vinapatikana. Kutokana na maandalizi niliofanya nguvu zimenishia, nahitaji mshirika tufanye ubia tuendeleze na kukuza biashara hii, Mambo yote safi anaehitaji ushirika pm wacha namba tuwasiliane.
 
Eneo lako ni kubwa kiasi gani?
 
mkuu nashauri ukomae tu mwenyew taratibu,kwa hatua uliyofikia umejitahid sana na itakuwa ngumu kuwa sawa na mshirika atakaejitokeza sabab hamkuwa na maono ya pamoja ya hyo project toka mwanzo.
 
mkuu nashauri ukomae tu mwenyew taratibu,kwa hatua uliyofikia umejitahid sana na itakuwa ngumu kuwa sawa na mshirika atakaejitokeza sabab hamkuwa na maono ya pamoja ya hyo project toka mwanzo.

Wazo zuri mkuu lakini uendeshaji kwa sasa unasuasua kasi ndogo. Nataka mshirika atie kasi tusonge mbele
 
mkuu inabidi uongezee taarifa muhimu mfano umeishatumia kiasi gani na unahitaji kurudishiwa au partner achangie consumables tu? Nini mission na vision zako mf mie na njaa yangu naweza kuja nikijua dividend ni baada ya miezi sita kumbe wewe una maono kila pato liingie kuitanua na kuikuza biashara. Na je una maono ya kuku tu au mifugo mingine kuleta flexibility na kupunguza kutegemea kitu kimoja tu? Projection zake mfano kila mwezi itatoa net kiasi gani? SWOTs?? Kipi cha kipekee, utofauti, kuvutia kuliko wafugaji wengine? Malori ya mayai huko? Umejipangaje kuhusu hili mf kupunguza gharama kwa kulima chakula chao mf mahindi? Si kuwa kwa undani lakini wadau waweze kuvutika. All the best
 
Bahati mbaya JF kuna like 1 tu, umeongea mambo ya msingi sana ambayo watu wengi wanajiingiza kwenye biashara bila kuwa na majibu ya hayo maswali na kujikuta wakifanikiwa kwa kubahatisha au wengine kupata hasara na kundi lingine kupata faida ya chini sana.

Darasa zuri sana, nafikiri Jogoo10 ataweka huo mchanganuo ili wanaotaka kuingia nae ubia wawe na habari za kutosha kuamua kufanya maamuzi sahihi na ikiwezekana kujiunga nae na kuboresha zaidi uendeshaji wa hiyo biashara! Ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:

ubarikiwe nawe pamoja mkuu. Hata nami nina mpango wa kitu kama hiki ingawa bado najipanga
 
Last edited by a moderator:
Iam intrested lakini kama mama joe alivyoelezea mkuu inabidi ufunguke zaidi
 
Nakushukuru mkuu samaritan, pia namshukuru sana mama joe kwa hoja zake. Ok kuhusu gharama kuanzia kiwanja, mabanda, vifaa na kuku wa kuanzia nimetua jumla sh milioni 25. Eneo ni heka 1. Mamajoe na wadau wengine nawakumbusha ufugaji ni kilimo kunahitajika mda wa mavuno, ila mimi tayari nimesha lima na kupanda na mbegu tayari zimesha ota ndipo uwezo ulipo nishia nahitaji mshirika apalilie ili tuvune. Uendeshaji wa mradi hadi kufikia kujitegemea inahitaji mda wa miezi 12. Baada ya hapo biashara ya kuuza kuku, mayai, na vifaranga itaanza rasmi. Mradi utajitegemea na kuingiza mapato kila siku, zitatolewa gharama za uendeshaji na kuweka hakiba. Tukifikia hatua hiyo tutatoa gharama zetu tulizo anzishia mradi. Na mradi utabaki huru na kuendelea pia kujitanua zaidi wadau kumbukeni mradi ni kuku wakienyeji. Kuhusu kupunguza gharama sio kulima shamba la mahindi ni kuongeza sababu ulimaji kutegemea mvua za kawaida matatizo matupu. Cha kufanya ni kununua mazao kwa wakulima yanayo hitajika kutengenezea chakula cha kuku na baadhi ya vitu vingine halafu ni kujitengenezea chakula mwenyewe. Kwa mbinu hiyo unaweza kupunguza bei ya kuku, mayai, na vifaranga. Utajitengenezea soko zuri na kuwa tofauti na wafugaji wengine.mkuu samaritan na mama joe na wadau wengie na wajasiriamali wenzangu anaependa kujikita eneo hili asihofu nasema karibuni ni mp wacha namba nitakutafuta. Mbarikiwe sana.
 
mkuu maelezo yako hayajitosheleza unatakiwa kuchanganua hiyo Milioni 25 ilivyo tumika. kusema tu umetumia 25 milioni haitoshi, watu wanataka kuona ulivyo itumia.

Na ninavyo jua kama kuku ni wa mayai basi withini 6 month tiyari wanataga sasa hiyo ya miezi 12 ni kwa kuku wapi?

Na kama ni wa nyama basi ni chini ya hapo,

Halafu ni lazina ueleze unataka nguvu iongeswe kwenye wapi?
Na mwisho unajichanganya sana kwa sababu umedai wameanza kutaga tena baadae unasema miezi 12,

kushawishi mtu awekeze pesa yake si ishu ya kitoto hata kidogo unatakiwa kweli kuja na maelezi ya kuweza kushawishi mtu awekeze.
 
Na kama kuku ni wakienyeji sidhani kama wanahitaji gharama kubwa kiasi hicho.
 
Nakushukuru sana mkuu chasha ww ni mdau mzuri wa eneo hili sijui wapi panakukwaza. Usione mlioni 25 pesa nyingi ni ndogo sana kunulia aridhi, na kuanzisha majengo na kunulia vifaa mbalimbali na kuku wa kuanzia. Pia hapa mtandaoni hapamalizi kila kitu, nilicho fanya mimi nimetoa head line, pia fahamuoi hapa mtandaoni tunapashana habari wala sio mahali pa kupeana pesa. Swala la pesa litafuata pale tu atakae hitaji ushirika atapoliona eneo la mradi na kuafiki, ishitoshe pia mambo yote yataenda kisheria sasa wasiwasi upo wapi. Kuhusu miezi sita ya mradi haitoshi sababu kuku ni wachache inabidi wapate mzunguko wa miezi sita mingiene iwe 12 ili wazaliane litengenezwe kundi la kutosha ndipo biashara itapoanza rasmi. Mkuu chasha na wadau wengine karibuni eneo la mradi nahapo mkifika na kujionea ndipo mtapata mamuzi coz mchanuo wote mtaukuta live. Karibuni wote wapenda maendeleo. Na mbarikiwe wote mliopitia hapa asanteni
 
Ila ungekua wazi ingesaidia zaidi , Kuku wachache wangapi? gharama kwa siku wanatumia shilling ngapi? vile vile uwazi wako unaweza kusaidia ukapatiwa mawazo mazuri ukajikuta huhitaji tena mshiriki katika biashara yako
 
Nawashukuru wakuu wote mliopitia hapa na kuwacha michango yenu muhimu sitowasahau. Mkuu Malila, mkuu Wise-comedian, mkuu Mama Joe, mkuu Samaritan, mkuu Ameir,
mkuu Chasha poultry farm na mkuu Dampol. Kwaujumla wote nawashukuru sana napenda kuwajulisha mshirika tayari ameshapatikana tena hapa hapa Jf. Naishukuru sana Jf hakuna kinachoshindikana. Mbarikiwe wote idumu Jamii forum.
 
tunashukuru sana kwa uelewa wako na pia kupata mshirika hapa. Mungu azidi kuwasimamia na kuwaongoza. Bless
 
Nawashukuru wakuu wote mliopitia hapa na kuwacha michango yenu muhimu sitowasahau. Mkuu Malila, mkuu Wise-comedian, mkuu Mama Joe, mkuu Samaritan, mkuu Ameir,
mkuu Chasha poultry farm na mkuu Dampol. Kwaujumla wote nawashukuru sana napenda kuwajulisha mshirika tayari ameshapatikana tena hapa hapa Jf. Naishukuru sana Jf hakuna kinachoshindikana. Mbarikiwe wote idumu Jamii forum.

Nikushukuru kwa kurudi kutoa feedback,
Nitapenda kuja kuwatembelea hapo shambani kwenu kama mtakuwa tayari. Kuna kitu nataka kuona kwenu, na ndio maana nilikuuliza ukubwa wa shamba lako. Kuna kitu wafugaji wengi hasa tunaotaka kuja kuwa wafugaji wakubwa tunakisahau sana.
 
asante pia mkuu Jogoo10 kwa kutoa mrejesho,nawatakia mafanikio katika mradi wenu.
 
Mkuu Malila tupo pamoja nitarudi tena kuleta jina la mradi na contacts zake.
 
Back
Top Bottom