Natafuta mshirika(partner) wa biashara ya bucha

vinkg

Member
Joined
Apr 29, 2017
Posts
15
Reaction score
14
partiner awe na:
1. Mtaji kama million 2 kwa ajiri ya mtaji na vitendea kazi
2. Awe mkazi wa Daresalaam, mwenye ueledi na ushirikiano
MCHANGO WANGU
1. Eneo la butcher, ni kwenye uzio wa nyumba yangu unaoangalia barabara, kwa hiyo hamna kodi
2. Umeme na maji
3. Nitatafuta leseni
4. nitasimamia biashara na kutunza reclord/kumbukumbu za mauzo kila siku
5. Kutafuta tender za nyama
6. Ulinzi wa vitendea kazi
ENEO LILIPO
Liko Sinza A karibu na kituo cha Remi Sheikhlango road. Njia
panda ya barabara iendayo mlimani city karibu na kumbi za harusi.
SOKO
wakazi wa eneo hili, wapita njia, wakina mamanitilie, butcher huku ni chache na ziko mbali mbali wala masoko kwa hiyo biashara ipo
KUGAWANA FAIDA
Partiner atachukua nusu au zaidi kwa kadiri ya maelewano.
Mtaji na vitendea kazi itabaki mali ya partiner
MKATABA
Partner akipenda tunaweza andikiana kwa mwanasheria
MIMi
Ni mtumzima, chapakazi, mwadilifu nina elimu ya kutosha, nina family mke na watoto tunaishi wenyewe tu hapa nyumbani Sinza makazi ya kudumu. Mi origin yangu ni Tabora
MAWASILIANO
1. private message (pm)
2. simu rigo 0672355 voda 0754639615 (saa 2 asubuhi mpaka saa 11 na nusu jioni
karibuni sana na aksanteni.
 
ni biashara ya butcher au biashara ya butchery?
 
Mkuu idea yako nzuri nakutakia kila la khery
 
Nini tofauti kati ya biashara ya butchery na butcher????
Butchery= ni biashara ya kukatakata nyama na kuiuza
Butcher = ni mtu anayefanya hiyo biashara.

hivyo basi, wewe umesema kwenye kichwa cha habari ' Natafuta partiner wa biashara ya butcher" , kwa hiyo utakuwa unafanya biashara ya watu wanaouza nyama? kwasababu butcher ni mtu, ila butchery ndio either eneo la kufanyia hiyo shughuli, au ndio shughuli yenyewe ya kuuza nyama.

haya tuambie sasa, unatafuta partiner wa kufanay biashara ya nini? sema kwa nguvu watu wote wakusikie!
 
Aksante mkuu ni biashara ya butchery (kuuza nyama ya ngo'mbe). Tutaajiri muuzaji au kama partner ana uzoefu huo utakuwa pia mchango wake kudhi iti biashara
aksante karibuni!
 
Ukipata baada ya kuwekeza milioni 2 huwezi kumuona partner mzigo? ukanunua kisiri siri vitu kisha ukampa vitu vyake na hasijue anapereka wapi?

Natamani sana ila naogopa sijui kwanini.!! Ila hasipo jitokeza mtu ntatokea ngoja nijadili kwanza na mke wangu.
 
Ukijifanya mjuaji cku zote unaeza zeeka hivo hivo
 
Niko na baadhi ya vifaa tuwasiliane nikuuuzie bei nzuri.meza nzuri kubwa ya kukatia nyama ya chuma pamoja na nguzo za chuma za kutundika nyama.ziko ktk hali nzuri nilifunga biadhara yangu.
 
Mkuu mkataba utakulinda na vigezo kwenye mkataba vitazingatiwa.
tunaweza anza na mtaji mdogo na ukakua kadiri ya biashara inavyoendelea.
Usisiwe na shaka mimi ni mwaminifu na mcha Mungu pia dhuruma kwangu ni dhambi
nipigie simu kwa mawasiliano zaidi
aksante
 
Una nia ya kweli Mkuu, kama mpaka mwakani utakuwa hujapata mwekezaji nitakutafuta maana ndo nitakuwa nimepata pesa. Tena mimi ni Bwana Afya kabisa nitasaidia kufast track mambo yaende na kuepusha usumbufu
 
ni biashara ya butcher au biashara ya butchery?

sawa tushajua ni mjuzi wa kiingereza! lakini ni biashara ya kuuza nyama. Kama hukuona vizuri, kichwa cha habari kimeandikwa kwa kiswahili sio kiingereza!!! duh!!!!
 
Mkuu projected returns zikoje? Namaanisha makadirio ya faida atakayopata partner kwa mwezi ni kiasi gani...? kwa gharama za modern butchery naona kama huo mtaji ni kidogo au tayari ilikuwa butcher kabla? Maana vifaa tu na kukite geneza chumba kikizi vigezo vya duka la nyama inazidi hicho kiasi by far.
 
Ukijifanya mjuaji cku zote unaeza zeeka hivo hivo
kubali kufunzwa ili ubadilike. kwa akili yako kama nisingekubadilisha ungeandika bango la ajabu sana kwenye hiyo bucha yako. nimekutoa matongotongo ulitakiwa kushukuru pusi we.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…