Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?
"Msaidizi"..anyway..shida kwa wale wanaoishi ughaibuni (Ulaya na Marekani) plse wasiwapotoshe ukwli bana . Ukiachilia mbali mazingira mazuri ya kuishi na kupata kirahisi huduma nyingine za kijamii, kuhusu watoto ughaibuni wapo watummishi hao waitwa "Baby sitters, Nannies, chidren cares/minders etc" ambapo wanaangalia watoto kwa mshiko mkubwa tu na ni kazi ya heshima inafanywa na wenye elimu maalumu pia!!.
Achilia mbali pia kuwa wapo wazazi wengi wanafanaya kazi kwa shift ambapo wengine wanaweza kutumia muda fulani kukaa na watoto kwa kubadilisha au unaweza kumpeleka mtoto hata kwa rafiki/ndugu wa jirani wakati upo kazini akashinda huko (hayo hayapo Bongo)!!
Hata masuala mengine kama kazi za ndani, si rahisi sana kukuta mtu anaekaa ughaibuni akawa na familia kubwa inayohitaji majukumu ya mtu zaidi ya mmoja. Hata kupika au kufua ni kama mazoezi tu. Kila kitu kinaendeshwa kwa technolojia . Kama unatumia mashine ya kufulia kama NN, au jiko la Umme kama MMK, au iwapo una kula vyakula vya "super market" kama Ngoshwe..haihitaji kuwa na mtumishi wa ndani.
Nyumbani kazi za ndani ni nyingi sana..kama unatumia jiko la kuni, unahitaki mtu wa kutafuta kuni, ukitumia mkaa..mtu wa kununua mkaa na mafuta ya taa kila kukicha..watu wanafanya kazi mbali na nyumbani, usafiri unasumbua..unachelewa kurejea kupikia familia (watoto)..ukirejea pengine umeme hakuna..mboga hakuna, maduka wamefunga ...maji ya kupikia chakua hakuna ...nk nk. Hayo yote mtumishi anaweza kusaidia.
Binafsi naona kuwa na mtumishi wa ndani sio kasumba bali inalazimishwa na mazingira..ila kwa wale wasiokuwa na kazi (mama wa nyumbani) hapo itatia shaka.