Nilishawahi kufanya automation inayokaribia kufanana na yako. Ilikuwa simple desktop program ambayo unaipa excel file, inasoma values zake, kisha inazijaza kwenye software ya 3D modelling (Catia). Nilitumia Python. Nakumbuka package zake mbili Tkinter na PyAutoGUI.
Wazo langu kwako, kama tayari unajua ni kwa namna gani wahitaji automation tool yako ifanye kazi, tumia ChatGPT ikusaidie kuandika hiyo program. Ukiipa maelekezo vizuri, na ukawa mvumilivu kuifafanulia unapoona haijaelewa, utapata program nzuri tu.
Natumia sana ChatGPT kunitengezea script mbalimbali na workflows za github, kama ni ishu za mara moja tu.