Mkuu nimefurahia sana hili wazo lako, naamini utapata michango mizuri yenye kukupa mwanga jinsi gani ya kufanya pamoja na gharama zake.Habari wakuu,naomba mwongozo wenu ni wapi naweza kupata kampuni au mtu anayeweza kunichimbia visima kwa ajili ya umwagiliaji shambani,mahali ni Dodoma na kwa vile shamba hakuna umeme ningefurahi kutumia teknolojia ya jua au upepo kuendeshea pampu.Kama una uelewa wowote tafadhali nisaidie.Natanguliza shukrani
Way back 2002 tulichimba visima kama vitatu dsm jamaa nimisplace namba yake ila water table kwa dodoma iko mbali sana so check na wale wanaotumia machine pls.Enzi zile kwa machine kila ksima tulichimba kwa 3MILL inclusive of submersible pump installation ya 1HP.
Unaweza check na wale jamaa wa visima wapo maeneo ya kamata pale opposite na shop rite ila wana gharama sana
Mkuu inategemea how far the water table is, sababu kama ipo mbali huenda cost yake ikawa kubwa kiasi kwamba it is easier kuvuta maji from nearby water source..., lakini nadhani cheaper way ni water harvesting ambapo unaweza ukachimba na kutengeneza underground water tanks (mfano wa septic tanks au mabwawa ambayo mvua ikinyesha yanajaa; (I think that is cheaper)
anyway for types of dugs wells angalia hapa
Groundwater: Wells
Pia jinsi ya kutengeneza water pumping solar station
Build your own solar-powered water pumping station by Jeffrey Yago, P.E., CEM Issue #91
[
Hiyo ni initiative nzuri sana. Jamani na sisii tunaomba contact za hao wanaochimba visima. Naomba kuulizia kitu kingine kuna njia nyingine inaitwa drip irrigation ambapo waweza tumia hata maji ya mvua. Nimeona kuna baadhi wanatumia hii njia ila sijaifuatiliza kwa ukaribu zaidi.
kwa youtube unaweza ona mengi zaidi
YouTube - ‪A few drops for more crops‬‏
Na link nyingine hiyo hpo
YouTube - ‪Drip Irrigation Improves Africa Food Production‬‏
Naona kenya wanajitahidi sana kupromote irrigation schemes...ona link hizo
YouTube - ‪Bura scheme up and running‬‏
JAMANI TUJUZE ZAIDI JUU YA UCHIMBAJI WA HIVYO VISIMA
wakuu, nadhani hii mada hapa ni pana sana...... haiishii kwenye kuchimba kisima tuu ..... lazima tuangalie vitu kama.... je baada ya kuchimba kisima tunahifadhi maji kwa namna gani matanki ya ardhini (underground reservoir tanks) au suspended?au mabwawa (dam) ..... je technology gani na vifaa vyake itatumika kufanya umwagiliaji wa shamba hili ..? je miundo mbinu gani inayotakiwa..? na pia ni nishati gani itakayotumika kufanya umwagiliaji huu...? kumbuka ukichimba visima unahitaji pumps (submersible) na vifaa vingi vitumiavyo nishati ya umeme je kuna chanzo cha umeme unaokidhi mahitaji...?
kwa Kifupi unaweza kupoteza pesa nyingi kwa kuchimba kisima kwa kubaatisha tu na mwisho wa siku hukakuta hakina maji, Gharama za kuchimba kisima ni kubwa sana nadhani mita moja inaenda kwa dola 50 mpaka 100 inategemea na kampuni na mashine wanayotumia (RIG) na kisima kinaweza kwenda mpaka meta 100. kwa hiyo kwa bei ya 50$ (ambayo ni bei ya chini sana) kwa mita 100 ni almost 5000$ (1600x5000=8000000) hapo bila gharama za mobilization na cost zingine
Kitu cha muhimu ni kufanya survey ya maji, ili ujue acquifer hipo sehemu gani na wapi kuna posibility ya kupata maji, hiyo survey mara nyingi hufanywa na Geologists, Geophycists na HydroGeologists
Survey kwanza inaanza na
1) Magnetic Profiling -ambayo wanaangalia usumaku wa aina tofauti za miamba zilizopo chini ya ardhi in relation to the earth magnetic fields( hii ina cover eneo kubwa kiasi),
2) Electromagnetic Survey-Hapa ile sumaku iliyopimwa inahusishwa na umeme kuangalia kama kuna uhusiano wowote (Hapa pia inacover eneo kubwa)
3) Resistivity Survey- Zile sehemu zilizoonyesha kuwa kuna uhusiano wa Sumaku na Umeme unazipima kiukamilifu ili kujua kama kuna conductive media (Maji) chini ya Ardhi (Hii inacover eneo dogo kutokana na majibu ya 1 na 2), hii pia inakuonyesha kama maji yana chumvi ama yapo safi, mpaka hapa unaweza kujua kisima chako kitakuwaje, lakini kwa umakini zaidi wataalamu wanapenda kufanya njia ya nne pia
4) Vertical Electical Soundings (VES)- hii inaweza kupredict the actual depth ambayo unaweza kuyapata hayo maji na probably lateral distance, kwa hiyo hizo point zako hapo ulizozipata hapo juu (number 3) unaziprioritize hipi iwe ya kwanza kuchimbwa na expected depth
kwa hiyo ukishapata hiyo report ndio unaitafuta kampuni yako ya kuchimba ukiwa na uhakika wa >90%,
nimeshuhudia watu wengi wana chimba visima na kupoteza gharama nyingi bila kupata maji amakupata maji ambayo muda si mrefu huwa yanakauka
Unapozungumzia underground water basi inapaswa yawe maji yanayopatikana kwenye miamba chini ya Adrhi, uwepo wa maji juu haina maana hayo maji yapo mpaka chini
kama kunakutokuelewa mniulize tu, maana vitu vingine kuvielezakwa kiswahili ni ngumu mno
I can't explain how much I have appreciated your contribution boss,ni kweli kuna ulazima wa kufanya survey kabla ya kuchimba unaweza kujua walau cost za kufanya hiyo survey? na how surveyors naweza kuwapata wapi?
Nafikiri ungetaja walau cost za kusurvey na majina ya walau wadau watatu wanne/au kampuni zinazofanya survey ungekua umetusaidia sana na wengine tukajifunza kupitia hili somo linaloendelea hapa, ahsanteSasa hivi wapo wengi wanaofanya hiyo kazi japo poa wengi hawana uhakika kwa asilimia kubwa, eneo lako liko mahali gani?