kwa Kifupi unaweza kupoteza pesa nyingi kwa kuchimba kisima kwa kubaatisha tu na mwisho wa siku hukakuta hakina maji, Gharama za kuchimba kisima ni kubwa sana nadhani mita moja inaenda kwa dola 50 mpaka 100 inategemea na kampuni na mashine wanayotumia (RIG) na kisima kinaweza kwenda mpaka meta 100. kwa hiyo kwa bei ya 50$ (ambayo ni bei ya chini sana) kwa mita 100 ni almost 5000$ (1600x5000=8000000) hapo bila gharama za mobilization na cost zingine
Kitu cha muhimu ni kufanya survey ya maji, ili ujue acquifer hipo sehemu gani na wapi kuna posibility ya kupata maji, hiyo survey mara nyingi hufanywa na Geologists, Geophycists na HydroGeologists
Survey kwanza inaanza na
1) Magnetic Profiling -ambayo wanaangalia usumaku wa aina tofauti za miamba zilizopo chini ya ardhi in relation to the earth magnetic fields( hii ina cover eneo kubwa kiasi),
2) Electromagnetic Survey-Hapa ile sumaku iliyopimwa inahusishwa na umeme kuangalia kama kuna uhusiano wowote (Hapa pia inacover eneo kubwa)
3) Resistivity Survey- Zile sehemu zilizoonyesha kuwa kuna uhusiano wa Sumaku na Umeme unazipima kiukamilifu ili kujua kama kuna conductive media (Maji) chini ya Ardhi (Hii inacover eneo dogo kutokana na majibu ya 1 na 2), hii pia inakuonyesha kama maji yana chumvi ama yapo safi, mpaka hapa unaweza kujua kisima chako kitakuwaje, lakini kwa umakini zaidi wataalamu wanapenda kufanya njia ya nne pia
4) Vertical Electical Soundings (VES)- hii inaweza kupredict the actual depth ambayo unaweza kuyapata hayo maji na probably lateral distance, kwa hiyo hizo point zako hapo ulizozipata hapo juu (number 3) unaziprioritize hipi iwe ya kwanza kuchimbwa na expected depth
kwa hiyo ukishapata hiyo report ndio unaitafuta kampuni yako ya kuchimba ukiwa na uhakika wa >90%,
nimeshuhudia watu wengi wana chimba visima na kupoteza gharama nyingi bila kupata maji amakupata maji ambayo muda si mrefu huwa yanakauka
Unapozungumzia underground water basi inapaswa yawe maji yanayopatikana kwenye miamba chini ya Adrhi, uwepo wa maji juu haina maana hayo maji yapo mpaka chini
kama kunakutokuelewa mniulize tu, maana vitu vingine kuvielezakwa kiswahili ni ngumu mno