Natafuta mtaalamu wa mambo ya mahusiano, matatizo yangu ni makubwa, tafadhali nisaidieni

Jipe muda wa kusamehe ijapokuwa ni ngumu kusahau. kumwacha si solution maana hujui utakaekutana nae atakutenda mangapi mabaya zaidi. Hata mi nilipita stage hiyo na sasa nimejifunza kupenda tena kikawaida tu na si kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yanakwenda that all na watoto ni faraja tosha!
 
Ngoja nikwambie kitu kbla haujafanya yote hayo kumbuka milkutana mkiwa wawili na mkapendana na kukubaliana na hakuwepo mtu ila kwanza chukua hatua hii kabla haujafanya chochote kingine

1. Mweleze ukweli siku hizi unamchukia
kwa aliyoyafanya hapo nyuma na
imesababisha kupoteza upendo wote

2. Mwambie ukweli na kuwa yeye ni mume wako na hautamani kuachana naye na ndiyo maana unamwambia ili kujaribu kuokoa hali hiyo na mrudie hali ya mwanzo

3. Jaribu kuacha kufikiria mabaya 30
aliyowahi kuyafanya na kumbuka
yale 70 ambayo aliwahi kukufanyia na
hata kukuvutia mpaka akawa mume
wako.

Kwa msaada zaidi ni pm nitakupa namba zangu nitakusaidia na hata kuongea naye kwa akili itakapobidi bila kujua kuwa umemwanika hadharani. But kumbuka kumpenda mtu ni kuamua amua kumpenda mume wako kwa gharama yoyote ile
 
Kwa msaada zaidi ni pm nitakupa namba zangu nitakusaidia na hata kuongea naye kwa akili itakapobidi bila kujua kuwa umemwanika hadharani. But kumbuka kumpenda mtu ni kuamua amua kumpenda mume wako kwa gharama yoyote ile

Mkuu hapo yangu macho:mod: BT....pole sana cha muhimu ni kumsamehe na kujifunza kumpenda tena...............ni ngumu kwa uwezo wako binafsi mshirikishe Mungu
 
Jamani hata wewe best unanichana!? Sina nia mbaya si unajua tena kuna mambo mengine ni ya ndani sana siyo ya kuyaweka humu jamvini maana yataonyesha udhaifu na kuharibu badala ya kutengeneza na pia BW wangu usiwe na wasiwasi kama unaona hatari tutaenda mimi na wewe na hapata haribika jambo wewe si unaelewa mambo fulani ya ndani jamani!?
 
Dada kama kweli amejirekebisha nakuomba uendelee kuishi nae kama ndugu yako huku ukijifunza kumpenda upya na uome mungu sana kwani msaada wake ni wa muhimu nae hapendi mifarakano ya familia .
AU umepata mwingine? au unakusudia na wewe kubadili mboga? USIJIDANGANYE huwezi jua kama utapata mwingine mwema ni bora hili zimwi unalolijua kuliko usilolijua
Kama bado anakunyanyasa ningekwambia usepe lakini kama kweli amebadilika huenda ameshafunzwa na dunia huyo msamehe mujenge familia watu wengi ni wazinifu na ndoa nyingi zina mawibi mengine ni makubwa zaid ya hayo ,okoa jahazi lisizame mwaya
 
huyo bana baada ya kutangatanga sana yamemshinda huko ndo kama unavyomwona anajidai kondoo,i hate dat,pole we endelea na pilika zako bana.coz hiyo kashtukia staili wakati mziki umepita.
 
Ataacha wangapi jamani we kaka/dada? kama amejirudi abaki nae
vinginevyo ajue kwamba kiasi kikubwa cha wanaume ni wanyanyasaji na wanatoka nje ya ndoa(samahanini kwa kuwa bias,it might be I am wrong)

 
Asanteni sana kwa michango yenu.

1. Ni kweli tunaishi nyumba moja
2. Ni kweli kayumba kifedha sana kwa sasa zaidi hana ajira kwa sasa, mimi ninayo nzuri kuliko yeye and it has always been like that, mimi ndio provider mkuu wa family mara nyingi.
3.tuna watoto 2
4. Me in love with someone else?? not sure...
 
Reactions: Mbu

...haya,..kwa wakati wako, chukua karatasi na kalamu uchore msitari kati.

Upande wa shoto orodhesha sababu unazodhani zinakulazimu uendelee na hiyo ndoa.
Upande wa kulia, orodhesha sababu unazoamini ndoa yako imefikia tamati.

Upande utaokuwa na wingi wa sababu (za kutosha) ndio utaokusaidia kwenye maamuzi.
Kila la heri.
 
wewe una tatizo lingine kubwa saana..
nalo ni kutokuwa na uwezo wa kusamehe..
sio tu mumeo.hata ndugu zako pengine..
kuna ile hali ya kuufunga moyo watu fulani wakikuudhi,hata wakikuomba msamaha
unakubali mdomoni but moyoni umeshawatoa moja kwa moja...

halafu,je mumeo angekuwa na hali nzuri,ingekuwa rahisi kumsamehe????????

kweli unahitaji mtaalamu.
nenda hospitali ya tumaini,wanae mama mmoja wa kihindi,atakusadia
 

Nikiri kutoka moyoni kwamba nimevutiwa na ushauri wa huyu mtu. Anaonekana anaongea kitu anachokielewa vyema. Ni kweli kbs kwamba it is possible mkaanza tena upya and the advantage u have is the fact that u know each other well. Better the devil u know than an angel u dont know
 
Jaribu kwenda likizo peke yako au na watoto tu bila yeye.. ukiwa huko utapata nafasi nzuri ya kutafakari upya nini unataka katika maisha yako.
 
Pole sana, unahitaji muda wa evaluate maisha yako upya, kuna wakati mtu anatakiwa kufuata akili yake na sio moyo wake, wewe ndio mwenye maamuzi ya mwisho lakini mshirikishe sana Mungu kwa imani yako. Jisamehe na msamehe kwa faida ya moyo wako. By the way ni PM kwa mengine zaidi
 
POLE SANA,
ila hapo uliposema hata hujui ulimpendea nini?, du!! umedhuhirisha ni jinsi gani umemkinai
na chanzo cha wewe kumkinai ni kutokana na makosa aliyokufanyia mwanzo.
Nakubaliana na aliyesema chukua karatasi ,
chora line A na B ,
Upande mmoja orodhesha makosa yake yote,
na upande wa pili orodhesha mazuri yake,
yale yatakayokuwa mengi na ya msingi katika NDOA yenu,
na utakayoona yanawafaa basi yachukulie uamuzi.

Mapenzi kufifia katika ndoa ni jambo linalotokea mara nyingi,
ila mkizungumza kwa uwazi ,na mkifanya juhudi za kuyastawisha tena,
yanaendelea kukua na kustawi tena kwa afya nzuri zaidi.

sometimes kuwa pamoja 24/7 na mume/mke kunachosha,
kupeana muda wa kuwa mbali japo siku 2,kuna raha yake mkikumbukana na kubadilisha mazingira.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA UAMUZI WAKO.
 
Hello Asha Ngedere,

jitahidi kuwa mkweli kwani umetuma ombi lako la kuwa unahitaji mtaalamu wa mambo ya mahusiano uku hali ukijua kuwa unadanganya, kwa ufupi mtu ulie mtumia ombi lako namfahamu,

Na nillijaribu kuwasiliana nae ili aweze kukusaidia, ila nawe ulimwandikia e-mail, ila katika ombi lako ulikuwa umendanganya, mara miaka 10 mara 5. pia jinsia umedanganya,

kwa ufupi huna tatizo. acha kuumba matatizo.
 
Something somewhere is wrong, sijaandika mail yoyote.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…