Natafuta mtu wa kuendeleza project ya kilimo urgent!!

pmas

Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
18
Reaction score
2
Habari!!!
Natafuta mtu wa kuendeleza project niliyoianza ya kilimo (eka 10, kilimo cha umwagiliaji, Dakawa-Morogoro).
Mpaka sasa 85% ya shamba limeshalimwa, liko katika hatua ya upandaji! (lengo ilikuwa kupanda mahindi na kuuza kama mahindi mabichi)
SABABU
1.Kuna hela (running cost) inahitajika haraka ili kulipia mpira wa water pump kwa ajili ya kumwagilia na pia hela ya mafuta ambayo kwa sasa sina, hela ya uhakika nayotarajia kwa ajili ya mradi ni mpaka mwezi wa 11 mwanzoni(nitakuwa nimechelewa, makubaliano kuhusu matumizi ya shamba ni mwezi wa kwanza mwanzoni, mbegu niliyopanga kupanda ni ya miezi miwili na nusu)
2.Mwezi wa 11 nina project nyingine ya kilimo natakiwa kuanza, so gharama za uendeshaji zinaweza kuwa kubwa sana. Ni project kubwa zaidi, inahitaji maandalizi ya mapema.
Nina vibarua 4, vifaa vya kulimia na water pump, pia vibarua wanakaa shamba.
Kwa atakayekuwa tayari itabidi anunue mpira immediately, ili kuwahi upandaji uwe ndani ya muda. Water pump kama hana nitamkodishia. Pia naweza kuendelea kusimamia shamba na kuendelea kutumia vibarua wangu kwa makubaliano maalum.
Kingine, itabidi anilipie gharama za uendeshaji nilizotumia.
Kwa aliye tayari ani pm
Asante.
 
Ndugu zangu habari zenu, naomba mnifahamishe eka-10 ni sawa na square meter ngapi kwa hesabu ya Tanzania?.
 
Ndugu zangu habari zenu, naomba mnifahamishe eka-10 ni sawa na square meter ngapi kwa hesabu ya Tanzania?.

ekari 1 ina sqmt 4700 kama sikusei mkuu ...kama nimekosea ntakuwa nmekosea kdg sana
hapo zidishaa hiyo 4799*10=utapata jibu
 
ekari 1 ina sqmt 4700 kama sikusei mkuu ...kama nimekosea ntakuwa nmekosea kdg sana
hapo zidishaa hiyo 4799*10=utapata jibu


Mkuu Mrangi, asante sana, je hiyo ni square meter au square yadi?
 
ekari 1 ina sqmt 4700 kama sikusei mkuu ...kama nimekosea ntakuwa nmekosea kdg sana
hapo zidishaa hiyo 4799*10=utapata jibu

Hapana! Umekosea Mkuu! Ekari 1 inapimwa miguu 70*70 au 140*35 (hapo kwenye miguu mwanangu ni mita hizo). Hivyo ekari 1 ina sqm 4900.
 
Ekari1=sqm4049~sqm4000. Spacing ya mahindi recommended ni 0.6m each & 0.7m apart.
So hesabu kamili kujua atapata mahindi mangapi ni 4000sqm÷(0.6m×0.7m)×10=95238.
Kama atauza kila hindi kwa bei ya sh200 pale shamba utapata sh 19,047,600/= then deduct gharama za uendeshaji ambayo obviously haizidi milioni5.
 

nimeupenda huu mchanganuo
 

Pia mimi nimeupenda huu mchanganuo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…