Johnny Impact
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 5,502
- 9,070
Kwa hali yako upendo wa dhati unahitajika kuliko hata hivyo vigezo unavyotoa.Ni Positive lkn kiukweli sijavutiwa na ambao nimewaona... ndo maana nikabandika ten bandiko ili.
Kuna watu wamewakataa waume zao kwa kujua au kutojua. Utakuta mdada mrembo (hata hajaathirika na UKIMWI) anakutana na kijana mstaarabu na anataka kumuoa lkn utakuta mwanamke hamtaki kisa hana kazi, hajaendana na vigezo vyake kama umbo sura n.k, anamfanyia visa na dharau na mwisho wa siku kijana wa watu anaamua ajiondoke.
Mtoto wa kike anakutana na type ya mwanaume ambaye anamhitaji (Ana vigezo vyote) lkn utakuta jamaa hana mpango ni mtu wa hit and run, kitu kinapigwa na jamaa anakimbia. Binti wa watu anakutana na wanaume tofauti tofaut na mwisho wa siku anaweza kupewa ujauzito au ukimwi. Utakuta mwanamke keshazalishwa mpaka watoto 3 na kila mmoja na baba yake lkn hapo mwanzo alikuwa anachagua mwanaume wa type yake na wengine kujikuta wameshaambukizwa Ukimwi.
-Hapo ndipo huwa najiuliza, mnachobagua ni nini? hapa ni sawa na mtu anaku overtake halafu huko mbele anapata ajali na kavunja miguu yote. Ukimuuliza sbb ya kukimbiza gari kwa mwendo kasi haijui. Pole sana
Huo ukimwi wako ni wa kuzaliwa nao au ni wakuambukizwa kwa njia ya ngono? km uliambukizwa kwa njia ya ngono na type yako bado haujaipata pole sana.