Natafuta mume anayeishi na VVU

Nakumbuka rafiki yangu alipima siku mbili kabla ya ndoa. Ikagundulika bibi harusi mtarajiwa alikuwa Positive wakati rafiki yangu ni negative. Mimi nilikuwa ni Best Man, jamaa hakunieleza kabisa. Wakafunga ndoa. Baada ya miezi 6 bibi harusi alipata mkanda wa jeshi tumboni na mimba ikatoka. Kuuliza kulikoni, nikapata hiyo story na kuwa walielezwa kuwa wawe wanatumia condom, ila rafiki yangu uzalendo ulimshinda akapiga kavu kavu ndo bibie kupata mimba. Mungu mkubwa walipopima tena akawa ni negative, nikamkataza asiende peku, wakaanza condom.

Bibie alikuwa ameokoka na Pastor wao akawaeleza kuwa mtu kama umeokoka hutakiwi kutumia condom. Bibie akagangamala kuwa hawezi kukiuka neno la mungu na kuchukua condom zote akazitupa shimoni. Rafiki yangu akakataa kuwa hawezi kujiweka katika mdomo wa mamba, hali ikawa mbaya kiasi ikabidi watengane.

Ninavyoandika ni kuwa bibie alishazikwa miaka kadhaa na jamaa yangu alioa mwanamke mwingine na wana watoto wakubwa.

Ujumbe: acha kujidanganya kuwa kwa vile mwanamke au mwanaume ana tatizo basi mkioana maisha yatakuwa kama unavyotegemea
 
Mkuu 'Life is full of try and error by never fail to try'......uenda ntapatia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…