Natafuta mume wa maisha...!

ladywho

Senior Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
107
Reaction score
49
Ninatafuta mwanaume wa kuishi nae awe na miaka 35-45. Awe mrefu angalau fut 5"5, asiwe na kitambi, awe na elimu kuanzia form 6, awe na upeo wa kuchambua mambo mbalimbali ya kijamii (anaeweza kuargue ktk jambo lolote bila kukwazika) asiwe smoker wa cigarete au weed, asiwe mlevi (mnywaji sawa tu).

Mimi nina miaka 31, mrefu kidogo, umbo la wastani na ni mzuri (kawaida) sivuti wala situmii pombe, elimu yangu form 6. Am serious ktk hili jamani wale mnaofanyaga utani mpumzike khdogo! Hapa vigezo na masharti vitazingatiwa. Kwa maelezo zaidi ni PM au nitumie ujumbe cecybenson@hotmail.com.

ASANTENI.
 
Well presented! good luck gyal! na Mungu akubariki utafanikiwa bless!
 
Dada, ukishakuwa mchaguaji hivi utakosa mume milele. Acha free style whoever comes who knows to love be your mume. La sivyo utapata vijana wa mjini watatwanga kote kote kisha wanaishia.
 
Dada, ukishakuwa mchaguaji hivi utakosa mume milele. Acha free style whoever comes who knows to love be your mume. La sivyo utapata vijana wa mjini watatwanga kote kote kisha wanaishia.

Ni mtazamo wako tu. Asante kwa kuchangia
 
Google..cecy benson
Nitarudi baadae
OTIS
 
walevi umetunyanyapaa aisee. unajua natafuta mwanamke mwenye vigezo kama vyako? vigezo ulivyo taja ninavyo sema tatizo ni kwamba nakunywa hadi nakuwa tilalila. vipi naweza kukupm.
 
Nakutakia mafanikio mema katika kazi uliyojitia kuifanya. Lakini mimi naamini kuwa njia nzuri ya kutafuta mme ni kupitia kuomba kwa mwenyezi Mungu(kama unaamini juu ya Mungu), rejea kile mtumishi wa Ibrahimu alifanya katika kipindi ametumwa na Bwana wake kwenda kumchukulia mke mtoto wake(Isaka). Lakini kama huamini juu ya Mungu, naamini pia ya kwamba utapata mwanamme wa kukuoa na sio mme. Hasara ya kupata mwanamme wa kukuoa ni
1. Nyumba kutokuwa na amani ambayo Mungu aliiandaa kwa ajili ya wanandoa.
2. Furaha kukosekanA ndani ya nyumba? na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Nisikuchoshe kwa maneno mengi, lakini nihitimishe kwa kusema "I wish you a good luck".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Hapo kwenye RED hiyo nyumba unataka iwe ni ya malumbano ya Hoja? Interesting......
 
Ni vema ungepost reception yako kwanza! wengine hatuko interested sana na umri wala umbo. Reception kwanza!
 
Kila la kheri dada! Humu tupo watu wa aina nyingi na mtazamo tofauti pia, kwa iyo ukikutana na michango hasi wala usikate tamaa. Unapaswa kujua nini unatafuta na kuamini njia uliyoitumia ni sahihi kwako na usimame katika hilo. JF mi njia tu ya mawasiliano na haimaanishi atayejitokeza ndo moja kwa moja anakuwa mume, lazima utachukua muda kumthaminisha. So Mungu atakusaidia katika kila hatua, jipe moyo, endelea na maombi, endelea na safari.
 

Ni pm if ur serious....liame_charm@yahoo.com
 
Nisubiri hapo hapo nina 26yrs.So baada ya miaka tisa tutaoana baby
 
nimechunguza topics nyingi ni wanawake kutafuta wanaume kuliko the other way around...ni kwamba wanawake wengi wa humu JF ni ma singo ladies, wameachwa, hawashikiki au hawatamaniki kwa wanaume ni swali tu :gossip:
 
nimechunguza topics nyingi ni wanawake kutafuta wanaume kuliko the other way around...ni kwamba wanawake wengi wa humu JF ni ma singo ladies, wameachwa, hawashikiki au hawatamaniki kwa wanaume ni swali tu :gossip:

shosty we mbona mpana hivyo??!! wapo wengi na ndo zao, wachumba na wapenzi..

ladywho, goodluck mumie..uwe mwangalifu kumchunguza vyema mwanaume utakayekutana nae!!
 

Asante kwa mawazo/ushauri
 
Hapo kwenye RED hiyo nyumba unataka iwe ni ya malumbano ya Hoja? Interesting......

unajua kuna watu mnakuwa mnajadili mambo hata ya kawaida lakini anapenda mada iende anakotaka yeye mradi amedominate, ukiongea kinyume nae au kumkosoa uvumilivu humtoka na unakasirikiwa!
 

Ni mtazamo wako tu ndugu! Huyo mke wa Isaka alishuka toka mbinguni au alikuwa humu humu duniani ila yule mtumishi alimwambia Mungu vigezo na ishara zake na Mungu alitimiza? Dont tell me humu jf hakuna husband material men na pia Mungu hayupo humu Jf? I'm doing ths on my own risk anyway.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…