Natafuta mume

Natafuta mume

Wapendwa
Mimi ni mgeni kwenye jukwaa hili, pamoja na kujiunga ili kutoa mchango wangu katika hoja mbalimbali nimeona sio vibaya pia nikachukua fursa ya kutafuta mwenza wa maisha
sifa zangu;

  1. Nina umri wa miaka 37
  2. Sijawahi kuolewa wala sina mtoto
  3. Naishi Dar na ninajitegemea
  4. Ni mjasiriamali
  5. Nimelelewa kwenye familia ya Islam
  6. Elimu yangu ni kidato cha nne
  7. Nina mwili wa kawaida (sio masongange), rangi ya maji ya maharage
Napendelea Mweza ninaye muhitaji
  • Awe na miaka 45 na kuendelea
  • Akiwa na mtoto ni sawa; nipo tayari kumlea kama mwanangu
  • Asiwe kwenye Ndoa ila kama alisha wahi kuoa haina tatizo
  • Awe na kipato (mjasiriamali au ameajiriwa)
  • Awe najua dhamani ya mwanamke katika nyumba
Kwa aliye tayari karibu pm tuchati

Dah aisee nipo dah...nicheki fasta pm!
 
Mujahedeen
Hahaaa Mkuu acha utani
Siku zoote taarifa zina sema kuwa; wanawake ni wengi kuliko wanaume
Hivyo ni lazima tukubali kuwa, sio wote wataolewa/wataolewa kwa wakati sawa

Naunga hoja ya waislamu kuoa mke zaidi ya mmoja pale mazingira yanapo ruhusu ili kufanya dada zetu wote waingie kwenye ndoa salama
 
Allah akujaalie upate mume mumeo. Mm age yangu haija fika huko na nina mke.
 
Mkuu!
Huo umri namba tu, just ignore it.
Cha msingi kijana akupende, ajielewa na awe fighter wa maisha basi.
Masuala ya ku consider number utasugua sana.
 
Nina miaka 28, ila Najiuliza hiyo miaka 37 nitaifikia lini ili niweze kutimiza vigezo vyako.

Hii JF mbona inanitesa na vigezo vya umri.
 
Back
Top Bottom