Natafuta muwekezaji kwenye Biashara ya Photography, Video Production na Graphics Design

Professor X

Member
Joined
May 29, 2020
Posts
45
Reaction score
60
Mimi ni kijana wa kitanzania Lengo La Kuja hapa ni kuomba msaada wa uwekezaji katika biashara ya VIDEO PRODUCTIN, PHOTOSHOOT and GRAPHICS DESIGN ili aweze kusaidia upatikanaji wa vifaa vitakavyo wezesha kufanya kazi vyenye thamani ya shilingi 6M (Million Sita).

Mtaji wangu utakuwa ni Uaminifu, wazo, Nguvu ma Muda Halafu Boss yeye Atawekeza katika hii project alafu tupange , nikae kama Business partner (tufanye Kazi alafu tuwe tunagawana faida Kulingana na mzunguko wa biashara Katika Asilimia ) Au niwe mwajiliwa wake nikisimamia kila kitu katika kazi alafu ye anilipe mshahara wangu wa kila mwezi

1.Video Light kit

2.CAMERA Canon 60D 1,500,000 na Canon mark 3 5D

3.Boya mic

4.Speed light

5.Strobe

6.Background

7.lens

8.memorycard

9.Stand

10.Compute

11.Reflactor

12.Printer

KUHUSU MIMI

Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 23 Elimu yangu ni kidata cho sita (siyo kwamba nilifeli hapana nimeshindwa kwenda chuo kutokana na changamoto za kifedha kuzimudu) Ni mzaliwa wa MBEYA MJINI na ndipo ninapo ishi kwa sasa

UZOEFU WA KAZI

Ni Mjuzi wa maswala ya VIDEOGRAPHY, PHOTOGRAPHY, FILMMAKING, GRAPHICS DESIGN, STORY WRITTER, Nimejifunza aya kwa mda wa miaka mi nne sasa sijaingia darasani ila nimekuwa nikijufunza kutoka kwa watu mbali mbali wenye ujuzi na aya maswala na kwa hapa nilipo nimefika sehemu naweza fanya kitu mwenyewe kwa uzoefu nilio nao

MAWASILIANO YANGU

0743150860 Voda 0688176045 Airtel

Natangulisha shukurani zangu za zati kwenu
 
Nitumie portfolio yako.PM
 
Mkuu ungeambatanisha na baadhi ya kazi ulizokwisha fanya, itarahisisha kupata muwekezaji
Hapa ndo changamoto inapo kuja nimekuwa mwanafunzi wa hii fani na kusaidiana na watu tu katika kufanya kazi lakini mimi mwenyewe sina kazi nilio wahi fanya kasi ninazo fanya kwa sasa ni graphics na photshoot lakini nina ujuzi wa kutosha wa hayo niliyo yaolozesha hapo japo sina kazi nilio wahi fanya nikutokana na changamoto za vifaa .kama utapata mda pita insta #TeteMwamba
 
Jitahidi Kushiriki vizuri katika matukio ya kijamii. Huku ndipo connection zinapatikana kwa haraka.
Usisubiri kuambiwa nenda Kanisani.
Pub & restaurant by
Attend sherehe mbalimbali
We foc tu connection na kama utapata camera yako we zuga nayo itakutengenezea jina
 
Safi sana na kila la kheri kwenye tasnia (carrier) yako hiyo.

Ila kwa ushauri wangu nadhani ungejikita kwenye eneo hili la Video na Photograph na ufanye bidii uwe mahiri haswa...hapo naona umejumuisha 'storywriting' ingawa nadhani unamaanisha 'script writing'...si mbaya ingawa hili nalo ni eneo linalojitegemea na si kama wengi tunavyojaribu kulipa wepesi.

Ila kama pia unatamani kuwa Sript Writer basi ujue kuna kazi ya kufanya ili kupata umahiri huo tofauti na kutanguliza tu kipaji.

Pambania Video production uwe Mahiri kama kina Adam Juma n.k...then baadae unaongeza na hizo kada nyingine unazozitamani.
 
Asante mku ulichosema ni kweli huwa najitahidi kushiriki matukio mbali mbali, lakini changamoto imekuwa ni vifàa, umekutana na mtu anakwambia haàaaa ungekuwa na vifaa tungefanya kazi hapo cha zaidi unajitahidi tu kujenga ukaribu nae ujifunze mawili matatu ila changamoto kubwa kwa sasa upande wangu ni VIFÀA kwo yoyote aliye tayari ata kunidhamini , ntamlipa taratibu kuendana na mzunguko wa kazi
 
Shukrani mkuu hili nalo ntalifanyia kazi japo kwa upande wangu natamani kujikita sana na video and photo japo changamoto ndo izo ndogo ndogo vitendea kazi ila asante kwa ushauri mkuu
 
Ungenihusisha nia kama kunasehemu unakwama
Kama hujapata kazi basi vuta subira. Ndani ya mwezi huu nitakutafuta. Nina mpango wa kuingia kwenye hii industry. Ngoja nii save namba yako.

Napenda sana kufanya kazi na vijana wenye vipaji na wanao jitambua. Naamini na wewe utakua ni mmoja wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…