Natafuta mwanamke wa kuoa

Natafuta mwanamke wa kuoa

JOESKY

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
816
Reaction score
2,034
Habari zenu wanajukwaa?

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nipo Dodoma mjini. Nina shahada ya kwanza ya ualimu ila sijabahatika kuajiriwa. Natafuta mwanamke wa kuishi naye maisha ya ndoa awe ni mcha Mungu na awe na miaka kati ya 24 na 30.

Mwanamke mwenye mtoto mmoja anatakiwa awe na kazi yaani ameajiriwa au amejiajiri asiye na mtoto hata asipokuwa na kazi.

Sifa za ziada
.Awe mzuri kitabia
.Awe muwazi na mkweli
. Awe mvumilivu
.Awe na mapenzi ya dhati
 
Hatimaye kapatikana...jf forever
 
Unamaanisha hutokua tayari kuhudumia mama mwenye mtoto asiye na kazi, ila uko tayari kuhudumia asiye na mtoto? Aisee Sisi wenye 2 kids bila kazi ndo hata hatusogei kabisa🤔🤔
😂😭😭😭😭 pole lakini sijawanyanyapaa bali ni kwa vile sipendi mtoto ateseke uku mwanzoni tukiwa tunayajenga
 
Tafuta kazi ulishe wanao jamaa anakutaka wewe, wanao pambana nao mwenyewe
Ha ha ha unajua hamna kitu kibaya kama kulea mtoto wa mwanaume mwenzio halafu utasikia leo nampeleka huyu akaonane na baba yake daaa hapo tayari roho inajua tu anaenda kutumika huyu
 
Kwa unachofanya ni kama simba kwenda buchani kuomba nyama badala ya kutumia uwezo wake kuwinda.

Mwanaume unafeli wapi kuwinda mwanamke?! Watu huwa hadi wanahama mkoa na kusafiri kutafuta mwanamke atakae mfaa. We unaonesha hauna nia ndio maana unapata shida kupata mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wenzako nasikia wanasemaga hadi waone alipozikwa baba wa mtoto ndio wanaoa.

sijawahi kufuatilia maana hayanihusu hayo mambo
 
Habari zenu wanajukwaa?

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nipo Dodoma mjini. Nina shahada ya kwanza ya ualimu ila sijabahatika kuajiriwa. Natafuta mwanamke wa kuishi naye maisha ya ndoa awe ni mcha Mungu na awe na miaka kati ya 24 na 30.

Mwanamke mwenye mtoto mmoja anatakiwa awe na kazi yaani ameajiriwa au amejiajiri asiye na mtoto hata asipokuwa na kazi.

Sifa za ziada
.Awe mzuri kitabia
.Awe muwazi na mkweli
. Awe mvumilivu
.Awe na mapenzi ya dhati
Huku Jf. Mabandiko yapo mengi wanotafuta waume wa kuoa ? Je umeshayapitia yote ? Au ulitaka kuandika Bandiko la kwako na ww tena ujulikane ?
 
Kwa unachofanya ni kama simba kwenda buchani kuomba nyama badala ya kutumia uwezo wake kuwinda.

Mwanaume unafeli wapi kuwinda mwanamke?! Watu huwa hadi wanahama mkoa na kusafiri kutafuta mwanamke atakae mfaa. We unaonesha hauna nia ndio maana unapata shida kupata mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
hujaeleweka
 
Huku Jf. Mabandiko yapo mengi wanotafuta waume wa kuoa ? Je umeshayapitia yote ? Au ulitaka kuandika Bandiko la kwako na ww tena ujulikane ?
Kinachokutesa nini?
 
😂😭😭😭😭 pole lakini sijawanyanyapaa bali ni kwa vile sipendi mtoto ateseke uku mwanzoni tukiwa tunayajenga
Ni hivo kweli ama waogopa kuhudumia mtoto asiye wako mkuu. Nilitaka nikupe zawadi ya hawa watoto wangu ila basi tena🤔😜
 
Back
Top Bottom