Natafuta mwanamke wa kuoa!

expert2go

Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
28
Reaction score
6
Wana JR, niko hapa leo kutafuta mwanamke wa kuoa, ni kweli kwamba asilimia kubwa ya mahusiano yanayodumu au kukubalika ni kwa wale watu ambao wanafahamiana kwa muda mrefu, kwamba utamjua mtu anaishi wapi, wazazi wake, kabila, lake, dini yake nk, lakini ki-ukweli ukifuatilia vitu hivi, unaweza usipate mwenzi wako, kwani sio wote unao wafahamu wanafaa kuwa nawe ki-ndoa, hivyo basi kwa yule ambaye anaamini mtazamo wangu, tafadhari tuwasiliane, Ninahitaji mke wa kuoa ila awe anajua kusoma na kuandika, sijali kama uko divorced au single! Napenda mtu atakae weza ku-establish mapenzi upya kwa mtu mgeni from no-where! Please, tuwasiliane!

Kwa upande wangu, najua kusoma na kuandika, am a divorced man, nina mtoto mmoja wa kiume, ninafanya kazi, ninaishi Dar Es Salaam. Navuta sigara na nakunywa pombe lakini sio sana, niko tayari kubadilika kwa nitakaye kuwa naye kwa namna tutakavyokubaliana!
 
Mbona hujasema ATM yako ina kiasi gani?
 
Umri wako, una nyumba au umepanga?, kazi gani unafanya?, uko tayari kubadilika? kwa nini uliachika kwa mkeo?, mawasiliano ya mkeo uliyeachana naye yanahitajika, uko tayari kupima ukimwi?
 
Umri wako, una nyumba au umepanga?, kazi gani unafanya?, uko tayari kubadilika? kwa nini uliachika kwa mkeo?, mawasiliano ya mkeo uliyeachana naye yanahitajika, uko tayari kupima ukimwi?
Una maswali mengi!
 
Nikikwambia uache kuvuta sigara utakubali kuacha?

na huyo mwanaume atakayekukubalia kuacha sigara au kunywa pombe au kuacha kuangalia mpira ,,,,,,,,,,, huyo siyo mwanaume wa ukweli........... sioni msimamo mimi hapo.
 
Umri wako, una nyumba au umepanga?, kazi gani unafanya?, uko tayari kubadilika? kwa nini uliachika kwa mkeo?, mawasiliano ya mkeo uliyeachana naye yanahitajika, uko tayari kupima ukimwi?

gud qn! Haya njoo tujibie maswali haya
 
Unaacha vzri sana tu,tena wala sikulazimishi na wala hatugombani!
unaambiwa tu kwa upendo

yaani unikute navuta sigara , nakunywa alcohol , nawatch football............. umenikuta hivyo na ndivyo nilivyo halafu katikati ya mahusiano unaleta habari za kunibadilisha namna nilivyokuwa ( character yangu) , haiwezi kuwa fair kwakweli.
 
na huyo mwanaume atakayekukubalia kuacha sigara au kunywa pombe au kuacha kuangalia mpira ,,,,,,,,,,, huyo siyo mwanaume wa ukweli........... sioni msimamo mimi hapo.

Sioni kama kuna tatizo kubadilika kwa mwanamke/mwanaume umpendaye....!
 
Acha kuvuta sigara bwana, wanawake wengi hatupendi mwanaume anayevuta sigara.
 
Sijazaliwa nikiwa navuta sigara, hivyo hicho ni kitu knachowezekana asilimia mia!
 
Acha kuvuta sigara bwana, wanawake wengi hatupendi mwanaume anayevuta sigara.

Asante kwa ushauri, ila ni vizuri kuwa muwazi, sio baadae anakuja kulalamika hapa JF, weka vitu vyote wazi then baadae ikose sababu! Ila ki-ukweli sigara nimepunguza sana kasi, hivyo hata bila kuambiwa, ipo ktk plan ya kuisitisha!
 
Umri wako, una nyumba au umepanga?, kazi gani unafanya?, uko tayari kubadilika? kwa nini uliachika kwa mkeo?, mawasiliano ya mkeo uliyeachana naye yanahitajika, uko tayari kupima ukimwi?

Nimependa maswali haya, ila majibu yake ni person, atajibiwa yule ambaye atakuwa interested kunifahamu zaidi na maongezi ya ana kwa ana! nikiweka vyote hapa, je tukikutana tutaongea nini?!.. so, naamini nitakaye mpata atathibitisha hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…