RUBERTS
Senior Member
- Apr 5, 2012
- 136
- 50
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 41. Ninaye mtoto mmoja wa kike ana umri wa miaka 10. Tatizo ni kwamba mke wangu hashiki mimba nyingine. Tumeishaangaika vya kutosha kwa madaktari wa kawaida na waataalamu wa masuala ya wanawake (Gynoclogists) lakini naona hakuna uwezekano tena. Nimevumilia sana sasa naona nakata tamaa. Mimi nahitaji mtoto mwingine japo mmoja, lakini mke wangu hataki nizae nje ya ndoa. Sifa za mwanamke ninayemtaka ni hizi: Awe na kazi na elimu anglau form six, anaweza akawa na mtoto lakini si zaidi ya mmoja, awe mzuri na mweupe, dini siyo muhimu sana ila mimi ni mkristo, awe na uelewa wa kutosha wa maisha, asiwe na ugonjwa wa aina yoyote, awe mchangamfu, asiwe after money. Mtoto akizaliwa awe tayari kupima DNA ili kujihakikishia kuwa mtoto ni wangu. Maana matapeli wako wengi.