Natafuta mwanasheria atakae nisikiliza,bila malipo Mbeya

Natafuta mwanasheria atakae nisikiliza,bila malipo Mbeya

Chemist boy

Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
57
Reaction score
60
Habari wakuu.
Nahitaji mtu anejua sheria aliepo dar es salaam nikutane nae nimpe kesi nzima anisaidie maana naona sikutendewa haki.
 
Habari,Mimi nimefukuzwa kazi kampuni ya coca cola mbeya,ila nilipewa charge yenye mashtaka mawili,shitaka la kwanza kikao cha ndani kilinikuta sina kosa,shitaka la pili kimsingi lilizaliwa kutoka shitaka namba moja,wamenikuta na hatia,na kuniterminate,nahitaji mtu anaejua sheria aliepo mbeya nikutane nae nimpe kesi nzima anisaidie maana naona sikutendewa haki,chuki binafsi ili tumika,kwa sababu mgogoro ulishasuluhishwa na boss,ila kiongoz wangu akuridhika akanishitaki kwa afisa mwajiri ndipo hila ilipoanzia.
Weka hapa usaidiwe, hapa ndo bure.
 
Kuna jamaa humu lawyer atakusaidia ila jipange kutoa vihela kidogo
 
Huko mbeya hamna waganga, sametime kuna watu wanaboa..

kama boss amekuta huna kosa na kuyasuluhisha yakaisha huyo jamaa anataka nini tena? ngozi nyeusi sijui lini mtabadilika
 
Mzee we acha tu,historia f
Huko mbeya hamna waganga, sametime kuna watu wanaboa..

kama boss amekuta huna kosa na kuyasuluhisha yakaisha huyo jamaa anataka nini tena? ngozi nyeusi sijui lini mtabadilika
We acha tu mkuu,uyo HRO. amekuwa akifanya mambo anavotaka,amewahi kublock personal bank A/c ya mtu na hela ilikuwa blocked mda mrefu adi alipojisikia akaiachia kwa kubembelezwa sana
 
Acha kupoteza muda, unatakiwa kupeleka mgogoro wako Tume ya usuluhishi na uamuzi hapo mbeya ndani ya siku 30. Nakushauri ufike vyama vya wafanyakazi hasa TUICO. Siku 30 zikiisha una hatari ya kupoteza haki yako unayo iamini.
 
Ni

Nitafanye ivyo kiongozi
 
Pole mkuu utasaidiwa lakini kuna gharama kiasi hapo sio bure kabisa gharama za form ambazo utazipeleka kwa manager wa kampuni, kwa hiyo taasis ya TAHURA Tanzania human right foundation inatoa misaada mbari mbari km hiyo yako. na swala lako ni la CMA na sio high court njoo inbox no ni hii 0768 853 050 usibeep. Dispute hizo tulisha tatua ikiwemo coca cola mwnza, n.k taasisi hii inafanya kazi mikoa mingi ikiwemo mbeya karibu asante...#
 
Nakushauri uwatafute wale wanaomtetea Abdul Nondo,unaweza kupata msaada bila malipo yoyote, wanahusika na haki za binadamu/kiraia kama sikosei.

Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom