Hi guys ni matumaini yangu mko poa
Nimerudi tena hapa love connect,nataka kushare na wengi au wachache wenye kupenda maisha ya wengine
Kwa kipindi chote tokea nitoe tangazo hapa.Nimekuwa nikipata connection za watu wengi ambao wako -ve na ambao wako +ve
Nashukuru Mungu nimeweza kujisimamia,na kusimamia.Kuna wanaume walikuja kwa njia mbali mbali nili deal nao kwa namna ya wanavyokuja,wengine tuliishia kuchat tu maana aliekua anania alikua na subira na nilichukua takribani miezi 3 mpaka kuja kuonana
Wengi waliishia njiani,nilifanikiwa kupata wanaume 4 walio serious kwa dhamira zao lakini wawili walikua wana influence ya familia hawataki mkristo na mmoja hatukufanikisha wazazi wake walihitaji mwanamke wa kabila yake mmoja alisisitiza kuishi bila kuzaa maana alikua na watoto wawili.
Nilifanikiwa kupata wanaume 3 ambao walikuwa -ve na walikua tayari tuishi nilidhani ni uwongo na kujihakikishia tulienda kupima na nilijiridhisha walikua salama lakini kama awali nilitangulia nisingependa mtu aje kulia kwa ajili yangu hata kama aliamua yeye hivyo sikuwa na sababu ya kuendeleza mahusiano.
Pia nilipata wanaume 2 hawa walikua +ve ila hawakua tayari kushiriki mapenzi safe ili kutozalisha maambukizi mapya hivyo pia ilibidi tuishie tulipoishia nilichogundua watu wengi wanatatizo na watu wengi wamekata tamaa wengi wanasambaza virusi kwa makusudi inahitaji akili sana kupambanua mambo.
Kwangu mimi nimejifunza mengi maana nimejionea mengi lakini bado nadhani ninasafari ndefu ya kukamilisha ndoto zangu so nahitaji mtu wa kunyanyuka nae katika hali zote.
Kwa wale wenye tatizo kama yangu jitahidi kufanya selection at least upate mtu ambae anauelewa kuhusu VVU na awe na future bila kuangalia hayo unaweza kuishia kupata mambukizi mampya na lifetime stress wengi wetu tunakufa kwa stess na sio kirusi so watch out
Na wale mlio salama nawakumbusha play safe unaweza kuwa positive muda wowote onyesha upendo kwa victims muombe mungu sana
Mimi sikuzaliwa na ukimwi niliambukizwa na mama wa kambo kwa makusudi lakini nimesamehe na maisha yanaendelea na sihitaji kumuambukiza yeyote.
Asanteni