Natafuta mwanaume H.I.V Positive mrejesho

Natafuta mwanaume H.I.V Positive mrejesho

Kati ya hao wanaume watatu waliokuja kwako ambao ni -ve mmojawapo ni mimi!
 
thanks dear...hivi niwaulize watu wa mungu..bado kuna watu wanaamini unaweza kulogewa virusi vya ukimwi...kwa macho yangu nimekutana na familia moja..yani mtu anaumwa anakataa kwenda hospital,akalazimishwa akapelekwa kwa nguvu na akapimwa na kugundulika kuwa ni positive then ndugu waliompeleka hospitali hawaamini kama ndugu yao anaweza kuwa positive..wanahangaika kumpeleka kwa mganga..kweli jamani?

kiukweli elimu bado inahitajika sana..kwa matiki hii watu wengi watapotea just like that.

#be safe,no matter ur positive or negative
Pole sana mpendwa Mungu akupe haja ya moyo wako na azidi kukupigania.
 
Hongera sana kwa ujasiri ulio nao Mungu akupatie hitaji la moyo wako.
 
Hi guys ni matumaini yangu mko poa

Nimerudi tena hapa love connect,nataka kushare na wengi au wachache wenye kupenda maisha ya wengine

Kwa kipindi chote tokea nitoe tangazo hapa.Nimekuwa nikipata connection za watu wengi ambao wako -ve na ambao wako +ve

Nashukuru Mungu nimeweza kujisimamia,na kusimamia.Kuna wanaume walikuja kwa njia mbali mbali nili deal nao kwa namna ya wanavyokuja,wengine tuliishia kuchat tu maana aliekua anania alikua na subira na nilichukua takribani miezi 3 mpaka kuja kuonana

Wengi waliishia njiani,nilifanikiwa kupata wanaume 4 walio serious kwa dhamira zao lakini wawili walikua wana influence ya familia hawataki mkristo na mmoja hatukufanikisha wazazi wake walihitaji mwanamke wa kabila yake mmoja alisisitiza kuishi bila kuzaa maana alikua na watoto wawili.

Nilifanikiwa kupata wanaume 3 ambao walikuwa -ve na walikua tayari tuishi nilidhani ni uwongo na kujihakikishia tulienda kupima na nilijiridhisha walikua salama lakini kama awali nilitangulia nisingependa mtu aje kulia kwa ajili yangu hata kama aliamua yeye hivyo sikuwa na sababu ya kuendeleza mahusiano.

Pia nilipata wanaume 2 hawa walikua +ve ila hawakua tayari kushiriki mapenzi safe ili kutozalisha maambukizi mapya hivyo pia ilibidi tuishie tulipoishia nilichogundua watu wengi wanatatizo na watu wengi wamekata tamaa wengi wanasambaza virusi kwa makusudi inahitaji akili sana kupambanua mambo.

Kwangu mimi nimejifunza mengi maana nimejionea mengi lakini bado nadhani ninasafari ndefu ya kukamilisha ndoto zangu so nahitaji mtu wa kunyanyuka nae katika hali zote.

Kwa wale wenye tatizo kama yangu jitahidi kufanya selection at least upate mtu ambae anauelewa kuhusu VVU na awe na future bila kuangalia hayo unaweza kuishia kupata mambukizi mampya na lifetime stress wengi wetu tunakufa kwa stess na sio kirusi so watch out

Na wale mlio salama nawakumbusha play safe unaweza kuwa positive muda wowote onyesha upendo kwa victims muombe mungu sana

Mimi sikuzaliwa na ukimwi niliambukizwa na mama wa kambo kwa makusudi lakini nimesamehe na maisha yanaendelea na sihitaji kumuambukiza yeyote.

Asanteni
Dawa ipo nitafute
 
wadau..nikitaka kuelezea kila kitu sitafanya hata kazi zingine...najua wengine wanakejeli ila najua wapo wanaojifunza..niko kwa ajili ya kuwaelimisha wanaohitaji kujifunza kuhusu HIV..Kuna mdau anauliza ilikuaje nikaambukizwa na mama wa kambo...ni hivi nilianza kulelewa na mama wa kambo nikiwa dogo sana kama age of 6...mbaya zaidi alikua hatupendi,and baba hakua anatusikiliza that time even nyumba haikua na amani so baba hakuwa mtu wa kukaa home..ilienda mama akapata maambukizi hiyo ndio ilikua mbaya baba na mama hawakua na maelewano kabisa..nilikua na wadogo zangu 2 ambao walizaliwa negative..kutokana na migogoro ya home baba hakuwa akimuelewa mama..ilifikia hatua mbaya mama akawa anaumwa sisi ndio tunamuuhudumia..kuna siku alimwambia baba kama anamtenga atakufa na watoto wote...so alifanikiwa hilo alituchanja akatuambukiza...kwa akili za kitoto hatukujua kinachoendelea...alipofariki wadogo zangu walianza kuugua...tukapimwa and walikua positive..the story began...kuikweli hua sitamani kuikubuka hii story but nimeshare mjifunze...hapo nimeifaya fupi tu...kwenye family kuna issue nyingi ndugu zangu...kila wakati nawaambia ukimuona mtu positive msidhani kaikota kwa kupenda..No

jitathimini kama wewe ndio mimi unafanyaje?

umezaliwa mzima..leo niko hivi sio kwa kupenda nimeambukizawa makusudi...

mama yangu mzazi anaumia kiasi gani?

sometimes unakata tamaa..ila ukiangalia maisha ni yako unaamua kupambana

natamani nipate mtu atakae nionyesha nini maana ya mapenzi ninapokata tamaa..nataani nipate mtoto labda atanifariji napata na nani wengi ni waongo na wamekata tamaa..

ambao wanahitaji kuwa na mimi nawaonea huruma..

someone help..naandika hayo nikiwa na maauvu makubwa...yananiumiza
Kusoma Thread zako. Msomaji anaejielewa anajiweka ktk nafaci yako. Anaona kwa dhahiri moyo wako ulio jawa na ushujaaa.ila nafsi yako imekua dhaifu kwa maumivu ulioyapata... Nakusihi fanya maombi kwa wengi ili nafsi yako iwezeshwe na uendelee kuenshi na furaha.
 
Aseee nakuomba usikate tamaa ww bado ni mtu wa nguvu kabisa bado mungu anakupambania dada. Wapo negative lakin hawakutii maisha yako wewe
 
yes...mimi ni mfano hai...my viro load are undetected..kiasi kwamba nilipima juzi kazi dispensary wakaniambia sina virusi...nikachukua majibu huku nacheka...nadhani na kipimo chao kilikua kibovu..ndio maana wanasema test 3 times...if nimeenda na mtu si anajua niko okay...complicated
Nilidhani vile vipimo vina-check for antibodies na sio virusi vyenyewe, kwahiyo hata uwe na viral load ndogo kiasi gani bado kipimo kitaonyesha positive kwa sababu antibodies za HIV unazo ila viral load ipo chini. Hebu nieleweshe kidogo!
 
Back
Top Bottom