Natafuta mwekezaji (Investor) wa App yangu ya Online Casino

Bata Boy Official

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
259
Reaction score
309
Habari wakuu!
Mimi ni kijana ambaye ninatamani na ninapambana sana kuwa mjasiriamali upande wa mtandaoni (online au e-entrepreneur).

Miaka kadhaa iliyopita nilipata idea ya App ya Online casino (ambayo ni tofauti na online casino zilizoeleka kwa kila kitu),ila kwasababu idea kama idea haitoshi kushawishi mtu kuwekeza pesa yake kwako, nikaanza kuifanyia kazi, yaani kufanya designing ya UI (User Interface) nikatengeneza Wireframes lakini kama haitoshi nikatengeneza mpaka CLICKABLE-PROTOTYPE kabisa inayoonyesha utendaji kazi mzima wa App.

Hivyo sasa hatua iliyobakia ni ya kutengeneza App ili iweze kuanza kutumika rasmi yaani kuwafikia walaji.
Ila gharama ya kutengeneza Application ndio changamoto kwangu.
Nimeshafika sehemu mbalimbali kama Gaming Board pale posta, nimeenda Sportpesa kule Oysterbay, na sehemu nyingine mbalimbali kwaajil ya kufuatilia hiki ninachokiongelea hapa.

Sababu ya kufanya nije mpaka hapa jukwaani kuandika uzi huu ni kwamba, wenzetu wanasema "A problem shared,is a problem halved" wakimaanisha kwamba kushirikisha watu tatizo lako ni nusu ya kulitatua.

Sasa ninachowaomba wakuu kama unaweza kuwekeza au kudhamini App hii, au unafahamu mtu anayeweza kuwekeza au kudhamini, au hata kunielekeza sehemu ambayo ninaweza kupata uwekezaji au udhamini wa App hii, nitashukuru sana sana.

Endapo ukitaka maelezo zaidi kuhusu App hii, au kutaka kuona utendaji kazi wake nk tafadhali usisite kuja PM nitakupa mawasiliano yangu na taarifa zaidi ili tuyajenge.
Asanteni sana wakuu.
 
Tafuta Technical Founder na uandae pesa kadhaa ya kumlipa

Ila pia Online Casino nachojua sio tu suala la kuwa na App pia uwe na pesa ambazo utatumia Kama mtaji kuzungusha kwa Gambers
Mkuu hapo kwenye Technical founder sjaelewa unamaanisha App developer/programmer??
Na lengo la kuwa na huyu mtu ni lipi hasa?

Hapo kwenye pesa ya kuzungusha kwa Gamblers haina haja...ndo maana mwanzoni kabisa nilisema hii ni tofauti kabisa na online casino nyingine.
 
Sasa mtu atajuaje kama anaweza kukufadhili ikiwa hujasema unahitaji kiasi gani? Na utaelekezwa vipi kwa mfadhili ikiwa hatujui huyo mfadhili unamtaka awe na uchumi wa kiasi gani? nikuunganishe na Vodacom kumbe hela unayotaka unaweza kuipata kwa mwalimu wa sekondari tu?
 
Nimejaribu kuwasiliana na kampuni kadhaa za nje, gharama ya kutengeneza Online Casino App ni kati ya Tsh 50M na 90M
 
H

Hakuna mtu wakukupa pesa hiyo just kwakuwa na idea tu eti uneifanyia Ui excute kwanza uwe na MVP na deck ndio utafute huo uwekezaji
 
Dah yaani mkuu kamari Kama pombe siku hizi mnakuja na formula zenu wajanja mzidi kutuumiza [emoji23]
 
Mkuu amini kwamba hii ni tofauti kabisa na zilizoeleka, halafu hapana nakataa sio kuwaumiza, hii ni michezo ya kubahatisha, mwenye bahati ndiye mshindi na si vinginevyo, labda kwa makampuni mengine sijui.
 
H

Hakuna mtu wakukupa pesa hiyo just kwakuwa na idea tu eti uneifanyia Ui excute kwanza uwe na MVP na deck ndio utafute huo uwekezaji
Mkuu natamani ungefahamu namna nnavyoumia kufanya hatua hii maana ningesha program the whole App myself...lakini ndo hivyo Mungu anatupa Karama kwa kiasi chake.
Nashukuru lakini ni ushauri mzuri
 
Habari wakuu!
Mimi ni kijana ambaye ninatamani na ninapambana sana kuwa mjasiriamali upande wa mtandaoni (online au e-entrepreneur).

Miaka kadhaa iliyopita nilipata idea ya App ya Online casino (ambayo ni tofauti na online casino zilizoeleka kwa kila kitu),ila kwasababu idea kama idea haitoshi kushawishi mtu kuwekeza pesa yake kwako, nikaanza kuifanyia kazi, yaani kufanya designing ya UI (User Interface) nikatengeneza Wireframes lakini kama haitoshi nikatengeneza mpaka CLICKABLE-PROTOTYPE kabisa inayoonyesha utendaji kazi mzima wa App.

Hivyo sasa hatua iliyobakia ni ya kutengeneza App ili iweze kuanza kutumika rasmi yaani kuwafikia walaji.
Ila gharama ya kutengeneza Application ndio changamoto kwangu.
Nimeshafika sehemu mbalimbali kama Gaming Board pale posta, nimeenda Sportpesa kule Oysterbay, na sehemu nyingine mbalimbali kwaajil ya kufuatilia hiki ninachokiongelea hapa.

Sababu ya kufanya nije mpaka hapa jukwaani kuandika uzi huu ni kwamba, wenzetu wanasema "A problem shared,is a problem halved" wakimaanisha kwamba kushirikisha watu tatizo lako ni nusu ya kulitatua.

Sasa ninachowaomba wakuu kama unaweza kuwekeza au kudhamini App hii, au unafahamu mtu anayeweza kuwekeza au kudhamini, au hata kunielekeza sehemu ambayo ninaweza kupata uwekezaji au udhamini wa App hii, nitashukuru sana sana.

Endapo ukitaka maelezo zaidi kuhusu App hii, au kutaka kuona utendaji kazi wake nk tafadhali usisite kuja PM nitakupa mawasiliano yangu na taarifa zaidi ili tuyajenge.
Asanteni sana wakuu.
Nenda Sahara Ventures kwa Jumanne Mtambalike
 
Nimeshaanza kulifanyia kazi wazo lake, kuna website nimejiunga tayari kwaajili ya kupata watu wa aina hiyo.
Ila kama endapo kuna Technical founder au co-founder specifically unawafahamu tafadhali naomba nielekeze nitawatafuta right away.
 
Pia kama kuna mtu, unafahamu casinos (land based) na au wamiliki wake tafadhali naomba nijulishe.
Kama utakuwa tayari kuzunguka pamoja na mimi (japo sio tajiri) naweza kukupa walau hela ya soda.
Nahitaji sana hii App wakuu
 
Nenda Sahara Ventures kwa Jumanne Mtambalike
Mkuu....nilienda kama ulivyonishauri lakini kumbe wao wanataka mtu ambaye ashaanza kufanya kitu tayari kinaingiza chochote kitu ila anataka kupata wawekezaji ili kukuza biashara yake...
 
Back
Top Bottom